Habari za michezo

ISHU YA AUCHO YASHUSHA PRESHA YANGA…SASA NI UHAKIKA ASILIMIA ZOTE JAMBO LIPO….

admin September 16, 2022 6:00 pm


Kiungo wa kimataifa wa Yanga, Khalidi Aucho raia wa Uganda aliyepata majeraha juzi dhidi ya Mtibwa Sugar, anaendelea vizuri kwa mujibu wa daktari wa timu hiyo, Shecky Mngazija ambaye amesema anaweza kutumika hata wikiendi ijayo.

“Aucho amepata majeraha ya kawaida tu kwenye mchezo huo mguu ulishtuka tukaona tusiendelee kumuacha uwanjani kwasababu angeweza kupata majeraha makubwa zaidi, ndipo mwalimu akaona ambadilishe kwa ajili ya mapumziko.”

“Licha ya kupata jeraha hilo mpaka muda huu tunaozungumza Aucho anaendelea vizuri na analeta matumaini makubwa sana na mashabiki wasiwe na wasiwasi na kiungo huyo,” amesema Shecky Mngazija.

BAADA YA KUPITIA MAGUMU….RONALDO AWEKA REKODI MPYA ULAYA…APIGA GOLI LA 700 MAN UTD WAKIOSHA NYOTA …. MWAMBA HUYU HAPAA…NABI ACHEKELEA KOONI KISINDA KURUHUSIWA…BOSI SIMBA AIONYA YANGA KWA WASUDANI…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply