Habari za michezo

BAADA YA KISINDA KURUHUSIWA ….MAMBO YABADILIKA YANGA…NABI AIBUKA NA MSIMAMO HUU …

admin September 17, 2022 8:13 am


Siku moja baada ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kupitisha jina la winga wa Yanga, Tuisila Kisinda kocha Nasreddine Nabi amesema anatarajia mambo mazuri kutoka kwake.

TFF, wametoa taarifa hiyo jana usiku ikieleza kuwa wamepitisha jina la Kisinda kwenye usajili baada ya Yanga kumuhamisha, straika Lazarous Kambole  na nafasi yake kuchukuliwa na Kisinda ili kutimiza idadi ya wachezaji 12.

Nabi amesema kuruhusiwa kwa mchezaji huyo anaamini kuna kitu kitaongezeka ndani ya timu yake.

“Ni mchezaji mzuri natarajia ataendelea na kasi ile ile ataongeza kitu ndani ya timu na naamini atarudi kwenye ubora aliokuwa nao kabla ya kwenda Morocco,” alisema Nabi.

Kisinda aliyerejea Yanga kwa mkopo wa mwaka mmoja akitokea RS Berkane ya Morocco hapo awali alizuiliwa kucheza kwa kile kilichodaiwa Yanga ilitimiza idadi ya wachezaji wa kigeni (12) kabla ya ujio wa Mkongomani huyo.

PAMOJA NA KUFANYA VIZURI….SIMBA HAWANA IMANI NA MGUNDA…KUMBE MPAKA SASA ‘ANAPIGA DEIWAKA”… MBALI NA KUPIGWA JUZI…MWAKINYO AZIDI KUTAKATA DUNIANI….ISHU NZIMA IKO HIVI…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply