Home Habari za michezo RASMI…SIMBA WATANGAZA SIKU YA KUACHANA NA MGUNDA…ISHU YA KOCHA MPYA YAWEKWA WAZI…

RASMI…SIMBA WATANGAZA SIKU YA KUACHANA NA MGUNDA…ISHU YA KOCHA MPYA YAWEKWA WAZI…


Uongozi wa Simba umebainisha kuwa umempa Mkataba wa muda kocha Juma Mgunda na hatma yake ipo kwa kocha mpya ambaye atakuja kukinoa kikosi hicho hivi karibuni.

Mgunda amekabidhiwa timu na mabosi wa Simba SC baada ya kutangaza kuachana na Mserbia, Zoran Maki ambaye alikiongoza kikosi hicho kwenye mechi 2 za Ligi Kuu Bara na alishinda zote.

Muda mchache baada ya kuachana na Simba, Kocha Zoran Maki akatangazwa kuwa Kocha Mkuu wa Klabu ya Ittihad kutoka nchini Misri.

Tayari Mgunda amekiongoza kikosi cha Simba kwenye mechi mbili moja ya Ligi ya Mabingwa Afrika ilikuwa dhidi ya Big Bullets kwenye hatua ya awali na Simba ilishinda mabao 2-0 kisha mchezo wa pili wa ligi dhidi ya Tanzania Prisons Simba wakishindao bao 1-0

Kuhusu suala la kocha mpya, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa klabu hiyo, Ahmed Ally amesema kuwa kwa sasa kocha wa Simba ni Mgunda mpaka utaratibu utakapokamilika.

“Ipo wazi kabisa taarifa yetu kuhusu kocha mpya wa Simba ni kwamba Juma Mgunda amepewa mkataba wa kuwa kocha wa muda na hilo analifanya na matokeo yanaonekana kukiwa na taarifa nyingine tutazungumza,” .

SOMA NA HII  MASTAA SIMBA WAANZA KWA MAJANGA MSIMU HUU