Habari za michezo

BAADA YA BARCA KUBUGIZWA GOLI 3-1NA MADRID ….XAVI KAONA ISIWE TABU AISEE…KAAMUA KUTEMA ‘NYONGO’ MAZIMA…

admin October 17, 2022 5:08 pm

Kocha wa klabu ya Barcelona Xavi, amewaambia wachezaji wake wanahitaji kubadilika kama wanataka kushinda ubingwa wa La Liga msimu huu hiyo ni baada kupoteza mchezo wa El Clasico dhidi ya Real Madrid.

Kocha huyo wa klabu ya Barcelona ameoongea hayo baada ya kufungwa katika dimba la Santiago Bernabeu na Real Madrid kwa mabao 3-1 na kuwafanya Barcelona kuachia Uongozi wa Ligi hiyo ambayo walikua wanaongoza kwa tofauti ya magoli.

Xavi anawahitaji wachezaji wake kubadilika kuelekea michezo mingine kama kweli wana nia ya kua mabingwa wapya wa La liga msimu na kuupokonya ubingwa huo mikononi kwa Real Madrid ambao hawajapoteza mchezo wowote mpaka sasa msimu huu.

Gwiji huyo wa zamani wa klabu hiyo pia anaamini hawakutumia nafasi ambazo walizipata katika mchezo kitu ambacho wapinzani wao walikifanya kwa ufasaha na kuwafanya wao kutoka mikono mitupu katika mchezo huo.

Barcelona ya Xavi kwasasa inashika nafasi ya pili baada ya kupoteza mchezo wao wa kwanza msimu huu katika La liga lakini bado wana nafasi ya kufanya lolote msimu huu na kweza kuondoka na taji lolote.

JAMAA ASHINDA MAMILIONI YA MERIDANBET KUPITIA SIMU KITOCHI….MKEKA WAKE HUU HAPA… MAMBO YA MO DEWJI HUKO SIMBA NI KUFRU TUPU…MASTAA WAPAGAWA…MGUNDA ATAJIRIKA GHAFLA….

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply