Habari za michezo

WAKATI LEO NDIO LEO….MASTAA HAWA MUHIMU WA YANGA KUIKOSA SIMBA…NABI APAGAWA..

admin October 23, 2022 5:48 am

KIUNGO mchetuaji wa Yanga, Bernard Morrison leo ataukosa mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Simba unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa.

Pia Crispin Ngushi huyu naye anatarajiwa kuukosa mchezo wa kesho kwa kuwa hajawa fiti.

Sababu ya kukosekana kwenye mchezo huo ni kutokana na adhabu ambayo alipewa kutokana na kosa la kumkanyanga mchezaji wa Azam FC kwenye mchezo wa ligi walipotoshana nguvu kwa kufungana mabao 2-2.

Nasreddine Nabi, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa wachezaji wengine wapo tayari na mazoezi ya mwisho yataamua kikosi na wale ambao wataanza.

“Morrison atakosekana kwenye mchezo wetu  dhidi ya Simba kwa kuwa ana adhabu lakini wachezaji wengine wapo vizuri.

“Sure Boy yeye alikuwa anaumwa lakini amepona hivyo kuanza kwake pia itategemea mazoezi ya mwisho kuelekea kwenye mchezo dhidi ya Simba,” amesema Nabi.

KUELEKEA KARIAKOO DABI KESHO…MASAU BWIRE KAONA ISIWE TABU USHINDI KAUPELEKA HUKU… SIMBA WAPEWA SIRI ZA ‘UCHAWI’ WA FEI TOTO…WAAMBIWA JINSI UNAVYOTUMIKA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply