Kocha Msaidizi Simba SC
Habari za michezo

KISA SARE NA YANGA JANA…MGUNDA AIBUKA NA HAYA KWA WCHEZAJI SIMBA….

admin October 24, 2022 5:50 am

Kocha Mkuu wa Simba SC Juma Mgunda, amesema wachezaji walipambana wakati wote wa mchezo dhidi ya watani wao Yanga lakini hatukufanikiwa kupata alama tatu.

Mgunda amesema wachezaji walicheza vizuri na walijitoa mpaka tone la mwisho la jasho lakini siku zote mpira una matokeo matatu, ambapo wamepata alama moja hivyo watajipanga kwa mchezo ujao.

Mgunda ameongeza kuwa mapungufu yaliyojitokeza kwenye mchezo wa leo atayafanyia kazi mazoezini na mazuri atayaboresha ili mechi ijayo apate alama tatu.

“Wachezaji wamepambana muda wote, lengo lilikuwa ni kupata pointi tatu lakini haikuwa hivyo. Tuliingia kwa kujua utakuwa mchezo mgumu na tulijitahidi kuwadhibiti wapinzani.

“Katika mchezo wa leo kulikuwa na mazuri ambayo tutayaboresha ili tufanye vizuri mechi inayofuata na yale mapungufu tutayafanyia kazi mazoezini,” amesema Mgunda.

SIMBA YAWA ‘KIBOGOYO’ MBELE YA YANGA KWA SIKU 1,345…MANULA AOMBA MSAMAHA MSIMBAZI… ZA NDAANI KABISA….SIMBA NA AZAM ZATEGEA TAMKO LA YANGA KUHUSU NABI…AKIFUKUZWA TU WANAYE…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply