Habari za michezo

BREAKING NEWS….YANGA WATOA TAARIFA RASMI KUHUSU KUACHANA NA NABI…

admin October 25, 2022 6:16 pm

TAARIFA: Uongozi wa Yanga unapenda kuwataarifu mashabiki na Wanachama wake kuwa Nasreddin Nabi, bado ni kocha mkuu wa timu yetu.

Nabi alijiunga na Yanga April, 2021 na amekuwa na rekodi nzuri ya kuiongoza timu yetu kubeba Ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu uliopita, bila kupoteza.

Akizungumza na YANGA MEDIA, Mtendaji Mkuu wa Yanga, Andre Mtine amewaomba mashabiki na wanachama wa Yanga kufuatilia taarifa za uhakika za timu yao kupitia vyanzo rasmi vya habari vya klabu.

“Niwaombe mashabiki na wanachama wetu kuwa na utaratibu wa kufatilia taarifa za klabu yetu kutoka kwenye vyanzo vyetu vya habari.

“Tuna YANGA APP. Tuna Website ya Young Africans na kurasa zetu za mitandao ya kijamii ambazo zimekuwa zikitoa taarifa za klabu yetu na kwa wakati sahihi,” alisema Andre.

Uongozi unamtakia kila la kheri kocha Nabi na benchi lake la ufundi kwenye maandalizi ya mchezo wa kesho wa Ligi Kuu dhidi ya KMC utakaopigwa saa 1:00 jioni kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa.

WAKATI TETESI ZA KUFUKUZWA ZIKIWA BADO ZA MOTO..NABI HUYU HAPA AFUNGUKA KUHUSU SIMBA… WAKATI YANGA WAKIJIUMAUMA KWA NABI….SIMBA WAPANGA KUIFANYIA ‘JAMBO BAYA’ AZAM FC..

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply