Home Habari za michezo TANZANIA U-20 WAANZA SAFARI YA MATUMAINI KUFUZU AFCON….

TANZANIA U-20 WAANZA SAFARI YA MATUMAINI KUFUZU AFCON….

Kikosi cha Timu ya Taifa ya Wanaume chini ya miaka 20 ‘Ngorongoro Heroes’ kimeondoka leo Alhamis (Oktoba 27) kuelekea Sudan, kwenye michuano ya kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika (U-20 AFCON), kupitia Kanda ya Afrika Mashariki na Kati ‘CECAFA’.

Shirikisho la Soka nchini Tanzania ‘TFF’ imethibitisha kuondoka kwa kikosi cha ‘Ngorongoro Heroes’ kupitia kurasa zake za Mitandao ya kijamii.

Taarifa iliyochapishwa kwenye kurasa za TFF imeeleza: Timu ya Taifa ya wanaume U20 @ngorongoroheroes imeondoka leo kuelekea Sudan kwenye mashindano ya kufuzu AFCON Kanda ya CECAFA yatakayoanza Oktoba 28, 2022.

Katika Michuano ya kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika (U-20 AFCON), kupitia Kanda ya Afrika Mashariki na Kati ‘CECAFA’, Ngorongoro Heroes imepangwa Kundi B lenye timu za Uganda na Ethiopia huku Kundi A likiwa na timu za Sudan, Burundi, Sudan Kusini na Djibout.

Michauno hiyo imepangwa kuanza kesho Ijumaa (Oktoba 28) hadi Jumamosi (Novemba 11) katika Uwanja wa Al Hilal mjini Khartoum-Sudan.

Timu zitakzotinga Fainali katika ukanda wa ‘CECAFA’ zitafuzu moja kwa moja kucheza Fainali za Mataifa ya Afrika chini ya Umri wa miaka 20 zitakazopigwa nchini Misri mwaka 2023.

Timu zitakazofuzu hatua ya Nusu Fainali kwenye Fainali hizo za Afrika, zitakata tiketi ya kushiriki Fainali za Kombe la Dunia chini ya miaka 20 ‘FIFA U-20 World Cup’ zitakazounguruma Indonesia mwaka 2023.

SOMA NA HII  KISA USHIRIKI WA SIMBA LIGI YA MABINGWA...ZAKAZAKAZI NA MANARA WAUMBUANA INSTAGRAM...