Staa wa Yanga SC Makambo atakiwa na Coastal Union
Habari za michezo

KAZE: MAKAMBO HAMNA KITU SIKU HIZI…TULITAKA MAYELE APUMZIKE TU…

admin October 31, 2022 3:19 pm

Kocha Msaidizi wa Yanga Cedric Kaze amekiri mshambuliaji Heritier Makambo alikuwa chini ya kiwango katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Geita Gold

Hata hivyo Kaze amesema walilazimika kumtumia Makambo ili kumpumzisha Mayele ambaye alipata majeraha wakati wakijiandaa na mchezo dhidi ya KMC

“Ni kweli Makambo hakuwa katika kiwango bora leo lakini ilikuwa ni lazima tumtumie ili kumpa Mayele mapumziko. Mpango ulikuwa kumpa Mayele muda wa kucheza usiozidi dakika 25, anarejea kutoka kwenye majeruhi na tutahitaji kumtumia katika mechi ijayo,” alisema Kaze

Katika mechi mbili dhidi ya KMC na Geita Gold, Makambo amekosa umakini ambapo ameshindwa kutumia nafasi kadhaa za wazi

Makambo alikuwa kipenzi cha mashabiki wa Yanga, lakini sasa anahitaji kufanya kazi ya ziada katika viwanja vya mazoezi ili kurejea katika ubora wake wa zamani

Ikumbukwe Yanga itaongeza nguvu kwenye dirisha dogo, Yacouba Songne yuko tayari kurejea baada ya kupona majeraha.

PAMOJA NA KUWA NA KIWANGO CHA ‘PANDA SHUKA’…LUSAJO APATA WA KUMTETEA LIGI KUU… TAJIRIKA NA MECHI ZA KUAMUA NANI KUFUZU 16 BORA-UCL…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply