Home Habari za michezo A-Z JINSI YANGA WALIVYOIFANYIA ‘UNDAVA’ KMC JANA….MAMBO HAYAKUWA MARAHISI HIVYO…

A-Z JINSI YANGA WALIVYOIFANYIA ‘UNDAVA’ KMC JANA….MAMBO HAYAKUWA MARAHISI HIVYO…

Fei toto Yanga SC

BAO pekee la kiungo Feisal Salum alilofunga dakika ya 80 limetosha kuipa pointi tatu katika mchezo wao dhidi ya KMC.

Mchezo huo KMC ilitawala dakika 45 za kipindi cha kwanza na kufanya mashambulizi mengi langoni kwa Yanga licha ya kutoweka moira wavuni.

Kipindi cha pili Yanga ilifanya mabadiliko ya kuwatoa Bakari Mwamnyeto, Tuisila Kisinda na Dickson Ambundo huku wakiingia Feisal Salum, Jesus Moloko na Zawadi Mauya.

Mabadiliko hayo yalimfanya Bangala ambaye alianza kama kiungo arudi kwenye beki wa kati kucheza sambamba na Ibrahim Bacca.

Wakati huo huo Aziz Ki ambaye alianza kama mshambuliaji wa pili alienda kucheza winga ya kulia aliyokuwa anacheza Kisinda ma eneo la ushambuliaji alienda kucheza Feisal Salum.

Mabadiliko hayo yaliifanya Yanga ipeleke mashambulizi kwa spidi langoni kwa KMC tofauti na ilivyokuwa kipindi cha kwanza.

Dakika ya 55 Yanga ilitaka kupata bao la kuongoza baada ya Jesus Moloko kupiga shuti la juu juu lakini kipa David Kissu aliucheza na kuwa kon ma isiyokuw na faida.

Wakati huohuo Kelvin Kijiri alionyeshewa kadi ya njano baada ya muamuzi Hery Sasii kuonyesha amemfanyia madhambi Farid Mussa na kipa wao Kissu alionyeshewa kadi ya njano bada ya kuonekana anapoteza muda.

Dakika ya 59 Bigirimana wa Yanga alionyeshewa kadi ya njano baada ya kumfanyia madhambi Hance Masoud.

Mchezo kwenye kipindi cha pili uligeuka kucheza kwa kukamiana kwani walikuwa hawapeani nafasi kubwa ya kucheza.

Dakika ya 66 KMC nayo ilifanya mabadiliko ya kuwatoa Awesu Awesu Emmanuel Mvuyekure na nafasi zao waliingia Masoud Abdalah (Kabaye) na Daruesh Saliboko.

Mshambuliaji wa KMC, Matheo Anthony alikosa utulivu dakika ya 69 kuiandikia bao timu yake baada ya Makang’a kuoiga krosi na yeye kuubutua mpira ukienda nje.

Yanga ilijibu shambulizi dakika ya 74 baada ya Gael Bigirimana kupiga krosi na Makambo aliiunga kwa kichwa mpira ukagonga mwamba na mabeki wa KKMC wakauondoa.

KMC nayo ilijibu mapigo baada ya Daruesh Saliboko kumpigia pasi Matheo Anthony ambaye alifyatuka shuti lililoishiw mikononi mwa kipa Diara Djigui.

Yanga ilionyesha kuhitaji ushindi kwani dakika ya 78 ilimtoa Bigirimana na kuingia Denis Nkane, mabadiliko hayo yakimrejesha Feisal kwenye kiungo na Nkane kucheza ushambuliaji.

Dakika ya 80 Yanga ilipata bao la kuongoza baada ya kutokea piga nikupige langoni kwa KMC na Feisal alipiga mpira na kwenda wavuni.

Dakika ya 85 KMC iliwatoa Kelvin Kijiri na Styve Nzigamasabo na kuingia Boniphace Maganga na Waziri Junior.

SOMA NA HII  SIMBA YAWAITA YANGA DESEMBA 11 WAMALIZANE...NABI AWAPANGIA SAPRAIZI...MWANASPOTI....