Home Habari za michezo ARSENAL ‘KUFA NA MTU’ LEO…MAN UTD USO KWA USO NA MOYES..

ARSENAL ‘KUFA NA MTU’ LEO…MAN UTD USO KWA USO NA MOYES..

Baada ya kutopata ushindi katika mechi mbili mfululizo zilizopita za mashindano tofauti, Arsenal leo ina nafasi ya kupooza machungu wakati itakapoikaribisha Nottingham Forest katika Uwanja wa Emirates.

Sare ya bao 1-1 ugenini dhidi ya Southampton, Jumapili iliyopita iliifanya Arsenal iangushe pointi mbili muhimu ambazo ziliwapunguza kasi yao katika mbio za kuwania ubingwa wa Ligi Kuu ya England (EPL) msimu huu.

Siku nne baadaye, Arsenal ilijikuta ikipokea kichapo cha mabao 2-0 ugenini dhidi ya PSV Eindhoven, matokeo ambayo yaliwafanya washindwe kukata tiketi ya kutinga hatua inayofuata ya mashindano ya Europa League licha ya kuendelea kuongoza kundi A ikiwa na pointi 12.

Arsenal inafahamu fika kuwa kupoteza leo dhidi ya Nottingham Forest ambayo imetoka kupata ushindi wa kushtusha kwenye mchezo wake uliopita dhidi ya Liverpool ambapo ilishinda kwa bao 1-0.

Meneja wa Arsenal, Mikel Arteta alisema kuwa kupoteza mchezo dhidi ya Nottingham Forest leo ni matokeo ambayo hayatovumilika baada ya kuangusha pointi nne katika mechi mbili zilizopita.

“Hakuna muda wa kuombana msamaha sisi wenyewe. Tunatakiwa kufanya kweli. Jumapili tuna mechi muhimu sana (dhidi ya Nottingham) na baada ya hapo tuangalie Zurich.

“Tunatakiwa kuwa bora zaidi ya tulivyokuwa (dhidi ya PSV). Tulijua nini wanachojaribu kukifanya na njia za kutimiza baadhi ya matendo. Namna tulivyo shindana, haikuwa vizuri kiasi cha kutosha,” alisema Arteta.

Mchezo huo dhidi ya Nottingham Forest leo utakuwa ni wa 200 kwa kiungo na nahodha msaidizi wa Arsenal, Granit Xhaka katika Ligi Kuu ya England.

Kwenye Uwanja wa Old Trafford, wenyeji Manchester United wataikaribisha West Ham United inayonolewa na kocha wao wa zamani, David Moyes wakiwa na kiu ya kuendeleza rekodi yao ya kutopoteza mechi kufikia michezo nane.

West Ham imekuwa haina mwenendo mzuri katika mechi za ugenini, jambo linaloweza kuwa faida kwa Manchester United ambapo katika mechi tano zilizopita walizocheza ugenini, wamepata ushindi mara moja tu huku wakitoka sare moja na kupoteza mechi tatu.

Kwingineko huko Hispania, Real Madrid itakuwa na kibarua cha kuendeleza rekodi yake ya kutopoteza mechi katika Ligi Kuu ya Hispania msimu huu wakati watakapokuwa nyumba kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu kuikaribisha Girona.

SOMA NA HII  REFA MECHI YA SIMBA SC VS HOROYA AC...KAMA YUPO FEA FEA VILEE...MNYAMA ASHINDWE YEYE KWA MKAPA