Home Habari za michezo DAKIKA CHACHE KABLA YA KUKIPIGA SUDAN…MAYELE AFUNGUKA ALIVYOMTAMBIA IBENGE…”NITAMFUNGA TENA”…

DAKIKA CHACHE KABLA YA KUKIPIGA SUDAN…MAYELE AFUNGUKA ALIVYOMTAMBIA IBENGE…”NITAMFUNGA TENA”…

Straika kiongozi wa Yanga SC, Fiston Mayele amesema wachezaji na bechi la ufundi la timu hiyo wameyasikia maneno kutoka kwa mashabiki na wanachama wa timu hiyo kuelekea mechi yao ya mkondo wa pili wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi Al Hilal ya Sudan itakayochezwa usiku huu.

Mayele amesema hayo akiwa Addis Ababa nchini Ethiopia pamoja na kikosi cha wachezaji wenzake 24 wakielekea Khartoum-Sudan kwa ajili mchezo huo kama wachezaji hawana jingine zaidi ya kupata ushindi katika mechi hiyo.

“Kabla ya mechi ya mkondo wa kwanza, niliongea na kocha Frolent Ibenge nikamwambia lazima nitamfunga mechi zote mbili, kwetu Dar es Salaam, Kwa Mkapa na nyumbani kwake Khartoum-Sudan. Sasa ya Dar nilimfunga na sasa nakwenda kumalizia kwake.

“Tunajua mechi itakuwa ngumu lakini tutahakikisha tunapata ushindi na kusonga mbele katika hatua ya makundi.

“Straika wake Makabi Lilepo ni mchezaji mzuri, ana kasi na akili ya mpira. Mechi ya Dar alikabwa vizuri na Djuma Shaban kipindi cha kwanza lakini kipindi cha pili nikaona amepelekwa katikati, alianza kusumbua akawa anapiga mipira mirefu.

“Tunafahama mchezo wa kesho atakuwa nyumbani, atataka kucheza ili kuwaonyesha mashabiki zake kwamba yeye i Mkongo na ana uwezo, lakini kwa upande wetu tumejipanga kupata matokeo, hakuna kingine zaidi Wanayanga wategemee ushindi,” amesema Mayele.

SOMA NA HII  BAADA YA KOSAKOSA ZA MAGOLI KUWA NYINGI....GOMES AFUNGUKA HAYA KUHUSU MUGALU