Home Habari za michezo RASMI….BAADA YA KUIKAMIA SANA SIMBA…MAYELE NA WENZAKE KUIKOSA GEITA LEO…

RASMI….BAADA YA KUIKAMIA SANA SIMBA…MAYELE NA WENZAKE KUIKOSA GEITA LEO…

Wachezaji watatu muhimu wa kikosi cha kwanza cha Yanga, Fiston Mayele, Joyce Lomalisa na Djuma Shaban wako njia panda kuwa sehemu ya mchezo wa leo dhidi ya Geita Gold kutokana na majeraha yanayowasumbua.

Mayele na Lomalisa hawakuwepo kwenye mchezo uliopita dhidi ya KMC walioibuka na ushindi wa bao 1-0 lililofungwa na Feisal Salum.

Kocha Msaidizi wa Yanga, Cedrik Kaze amesema bado benchi la ufundi halina uhakika kama nyota hao watakuwa fiti na kujumuishwa kwenye kikosi ama la ambapo walitumia mazoezi ya mwisho yaliyofanyika  jana jioni kufanya maamuzi juu ya hatma yao.

Kaze amesema kitendo cha kucheza mechi nyingi mfululizo na kwa kufuatana kinasababisha majeraha kwenye kikosi hali ambayo inalilazimu benchi la ufundi kufanya mzunguko wa wachezaji ili kukidhi mahitaji lakini akawatoa wasiwasi mashabiki wa timu hiyo kwani Yanga ina kikosi kikubwa ambacho kila mchezaji ana wajibu wa kuisaidia timu kupata matokeo.

Mbali na nyota hao watatu, Kaze amesema nahodha wa timu hiyo, Bakari Mwamnyeto ambaye ana matatizo ya kifamilia na Khalid Aucho anayeuguza majeraha ndiyo wachezaji pekee kwa sasa watakaoukosa mchezo huo.

“Ni kweli tumepata muda mchache wa kupumzika tumecheza michezo karibu minne ndiyo maana tunapumzisha baadhi ya wachezaji ikiwa ni jitihada ya kulinda utimamu wao, lakini hatufanyi mabadiliko ilimradi bali yatakayoleta mchango chanya,”

“Mwamnyeto na Aucho watakosekana
wengine wangali wanarudi kwenye kikosi mazoezi ya leo tutaona kama wataweza kutumika kesho (Mayele, Lomalisa na Djuma Shabani),” amesema Kaze.

Akizungumzia mchezo huo kwenye mkutano na waandishi wa habari, Kaze amesema wanaitambua Geita Gold ni timu bora yenye mwendelezo mzuri wa matokeo lakini wanapaswa kutetea nafasi yao na kuendelea kuwa kwenye nafasi kubwa ya kubeba ubingwa.

“Toka mwaka jana mchezo na Geita haujawa rahisi tunajua ni mchezo mgumu wana wachezaji wenye uzoefu wa ligi lakini tunapaswa kutetea nafasi yetu itakuwa mechi ya physical kwahiyo tumejiandaa, tunapaswa kuingia kwenye mchezo wa kesho na nguvu kubwa na kujitoa ili tupate alama tatu muhimu,”

“Objective yetu siyo kuwa na namba kubwa ya michezo ambayo ni unbeaten, sisi tunataka kuingia na uthubutu wa kupata ushindi na kutimiza malengo, tunaingia kwenye huu mchezo na nguvu kubwa sana kwa sababu tunataka kubeba makombe,” amesema Kaze.

Nyota wa Yanga, Denis Nkane amesema licha ya ratiba kuwabana watahakikisha wanafanya vizuri na kupata alama tatu kila mchezo huku akisema hawana presha ya kupata ‘unbeaten’ bali kusimama kwenye malengo na kutimiza yale waliyojiwekea.

SOMA NA HII  MWAMBUSI: KOCHA WA MAKIPA AMEPATIKANA