Habari za Yanga
Habari za michezo

BAADA YA KUGUNDUA MAYELE ATAKUWEPO KESHO…WATUNISIA WAANZA MBAMBAMBA ZAO MAPEMA…KOCHA WAO ALIA…

admin November 1, 2022 7:16 pm

Kocha Mkuu wa Club Africain, Bertrand Marchand amesema moja ya staa wa Yanga anayemuhofia katika mchezo wa kesho wa mchujo kwenye Kombe la Shirikisho Afrika ni Fiston Mayele.

Kwenye kikosi cha Yanga, Mayele ndiye kinara wa mabao kwenye Kombe la Afrika baada ya nyota huyo kutupia jumla ya mabao saba katika hatua zilizopita dhidi ya Zalan kutoka Sudan Kusini na Al Hilal ya Sudan.

Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam, Marchand amesema Mayele ni mchezaji mzuri ambaye anamfahamu kwa muda mrefu tangu akiitumikia AS Vita ya kwao DR Congo.

“Wakati nipo klabu nyingine kabla ya hii miaka miwili nyuma nilihitaji kumsajili kwa sababu alinivutia sana kutokana na aina ya uchezaji wake ila bahati mbaya sikufanikiwa kwa hilo.” alisema Marchand.

Marchand aliongeza mbali na Mayele ila pia anawafahamu Tuisila Kisinda na Jesus Moloko japo Yanga ina wachezaji wazuri kutoka mataifa mbalimbali hivyo ni lazima wajiandae vizuri kutokana na ugumu wenyewe wa mchezo.

WAMISRI WAPAGAWA NA MUONEKANO WA LIGI YA BONGO…WATOA SHINIKIZO HILI… KUELEKEA MECHI YA KESHO…NABI ATOA KISINGIZIO MAPEMA….AWATUPIA LAWAMA TFF KWA ‘KUMSINCHI’…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply