Habari za michezo

CHAMA: MOYO WANGU UMEYEYUKA …

admin November 7, 2022 2:39 pm

Kiungo fundi wa klabu ya Simba na timu ya Taifa ya Zambia Claotus Chama amefanikiwa kukutana na shabiki wake kijana mdogo anaefahamika kwa jina la Masanja aliejichora jina la kiungo huyo mkononi mwake.

Kijana huyo anaelelewa kwenye kituo cha kulelea watoto yatima kinachopatikana katika wilaya ya Kisarawe Mkoani Pwani, Siku kadhaa nyuma picha yake ilisambazaa kwenye mitandao ya kijamii akiwa amejichora tattoo ya kiungo huyo na kusema anammpenda sana.

Jana Chama ameweza kuweka picha kwenye mitandao yake ya kijamii ya Twitter na Instagram akiwa amekutana na kijana huyo mdogo ambaye ameonesha mapenzi makubwa na kiungo huyo wa kimataifa wa Zambia.

“Baada ya muda mrefu, leo nimepata nafasi ya kumtembelea kijana wangu Masanja na familia yake huko Kisarawe. Sikupata njia sahihi ya kumuonesha heshima baada ya kuchora jina langu mkononi mwake”

“Moyo wangu umeyeyuka kutokana na mapokezi niliyoyapata bila kusahau mazungumzo ya dhati baina yetu na familia yake. Nimefurahishwa sana nasubiri kuwaonesha safari ilivyokwenda” Aliandika Chama kwenye mitandao yake ya Kijamii

Wadau wengi wa mpira wa miguu wamefurahishwa na kitendo cha kiungo huyo kwenda kumtembelea shabiki yake na kumpongeza kutokana na mapenzi makubwa aliyoyaonesha kwa kijana Masanja.

MIKAKATI YA SIMBA QUEENS KUWA MABINGWA AFRIKA YAANZIA NA ‘MADEMU’ WA SAUZI… HIZI HAPA SIKU 60 ZA NDOA YA MGUNDA NA SIMBA…KAWEKA NA KUVUNJA REKODI KIBAO ZA WAZUNGU…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply