Home Habari za michezo GSM ATUMIA NJIA YA MO DEWJI YANGA IFUZU MAKUNDI…MASTAA YANGA KULAMBA BINGO...

GSM ATUMIA NJIA YA MO DEWJI YANGA IFUZU MAKUNDI…MASTAA YANGA KULAMBA BINGO NONO…

Habari za Yanga

KUANZIA Saa 2: 00 usiku wa leo, macho yote ya mashabiki yatageukia Tunisia. Yanga itakuwa kwenye Uwanja wa Olimpiki wa Hammedi Agrebi kumalizana na wenyeji wao Club Africain.

Juzi walipotua Jiji la Tunis wakakuta rais wao Injinia Hersi Said anawasubiri lakini kuna ahadi nzito wamepewa wachezaji hao kama wakifanya kweli katika mchezo huo.

Hersi hakusafiri pamoja na timu hiyo wakati ikifika Tunisia na kwenda kuweka kambi Mji wa Sousse uliopo umbali wa kilometa 147 kufika Jiji la Tunis ambako mchezo huo utapigwa hapo.

Yanga iliweka kambi hapo ya siku mbili tangu walipowasili hapo Ijumaa Novemba 4 kisha wakatua Tunis juzi tayari kwa jana kufanya mazoezi ya mwisho katika uwanja wa mchezo kuelekea mechi hiyo ya Kombe la Shirikisho.

Hersi ametua Tunis akitokea Uturuki na kuongeza nguvu akiungana na mabosi wenzake wa kamati ya utendaji wakiwemo Munir Said aliyetangulia mapema huku Alexander Ngai naye akitua juzi mchana.

Taarifa kutoka kambini ni kwamba wachezaji wamepewa ahadi ya Sh 200 Milioni kama watapata sare yoyote ya mabao au ushindi utakaoipa timu hiyo tiketi ya kushiriki Kombe la Shirikisho hatua ya makundi.

Ahadi hiyo inaelezwa ni ya kamati ya mashindano ya timu hiyo chini ya Mwenyekiti wake Rodgers Gumbo, pia inaweza kuongezeka kutokana na fungu la Bilionea wao Ghalib Said Mohamed ‘GSM’ ikiwekwa siri kwanza akisubiri sapraisi ya wachezaji wake baada ya firimbi ya mwisho.

Aziz KI atia neno

Kiungo mshambuliaji wa timu hiyo, Stephane Aziz KI ameliambia Mwanaspoti kuwa wanautazama mchezo huo kwa umakini mkubwa na kwamba wamekutana na kuhamasishana juu ya umuhimu wa matokeo ya kushtua.

Aziz KI alipongeza jinsi walivyokimbilia Sousse akisema kambi yao imekuwa na manufaa kutokana na kutoa nafasi kwao kuzoea hali ya hewa pamoja na kujiweka sawa kisaikolojia.

“Tuna kiu kubwa ya ushindi katika,t unaongea sana kama wachezaji na kuhamasishana juu ya hii mechi na umuhimu wa kubadilisha kasi yetu kwasasa tutaingia na akili kubwa katika mechi hii,” alisema KI ambaye leo huenda akaanzia kucheza pembeni kulia akimuachia Feisal Salum kucheza nyuma ya mshambuliaji wa mwisho.

Kocha Nabi Mohamed alisema; “Nina marafiki hapa wamenipa taarifa za kutosha juu ya wapinzani wetu, nafahamu kwamba kwa jinsi walivyocheza mfumo wa kujilinda kuna wachezaji wawili nimeshatajiwa kwamba wanaweza kucheza kwenye mchezo ujao.”

“Sisi tutaingia kimkakati kutafuta ushindi wa kukabiliana na yoyote, watatumia sana mabeki wao wa pembeni na mawinga kutushambulia kwa nguvu kitu pekee kitakachotuweka salama ni jinsi tutakavyotekeleza majukumu ya kuzuia kwa kushirikiana na sio kwa wachache.

“Tunatakiwa tukabiliane na kasi yao kwa kuwa watahitaji sana bao la mapema kama tukifanikiwa kuhimili kasi hiyo kisha tukawa na akili kubwa ya kuwashambulia itakuwa mechi ngumu.”

SOMA NA HII  KELVIN JOHN KUIONGOZA TAIFA STARS...MSUVA,SAMATA,ZIMBWE JR WATEMWA