Habari za Yanga
Habari za michezo

BAADA YA KUWATUNGUA WAARABU JANA…RAIS SAMIA AWAPA KONGOLE YANGA….

admin November 10, 2022 4:06 pm

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, ameipongeza Klabu ya Yanga SC kwa kufanikiwa kuvuzu hatua ya Makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Kupitia ukurasa wake rasmi wa Twitter, Rais Samia ameweka ujumbe huo wa kongole mara tu baada ya Yanga SC kuwafunga Club Africain ya Tunisia goli 1-0 katika mchezo wa marudiano baada ya awali kupata sare ya 0-0 katika Uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar.

“Kongoole Yanga SC kwa ushindi na kufanikiwa kusonga mbele katika michuano ya soka la wanaume kwenye Kombe la Shirikisho Afrika, msimu wa 2022/2023. Nawatakia kila la kheri katika hatua inayofuata,” aliandika Rais Samia.

Mara ya mwisho Yanga kutinga hatua hiyo ya Makundi ya Shirikisho ilikuwa mwaka 2018 ambapo waliishia hatua hiyo baada ya kumaliza mechi zao na kushika mkia katika kundi lao.

PAMOJA NA YANGA KUFUZU MAKUNDI JANA..MSIMU UJAO ISHU YA TIMU NNE CAF ITAKUWA HIVI… NI MANDONGA TENA….SAFARI HII AIBUKA NA HII MPYA KUWAHI KUTOKEA..

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply