Habari za michezo
FT: SIMBA SC 1-0 IHEFU …SAKHO APIGA GOLI LA MSHINDO…AZAM FC WALITAMANI MECHI IISHE HARAKA…
admin
November 12, 2022
9:08 pm
Baada ya kutoka sare ya kufungana bao 1-1 na Singida Big Star,timu ya Simba SC imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Ihefu mchezo uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.
Simba ilipata bao la ushindi dakika ya 63 likifungwa na Pape Sakho bao lililodumu hadi dakika 90.
Kwa ushindi huo Simba imefikisha Pointi 21 nafasi ya pili baada ya kucheza mechi 10 huku Azam FC wakikwea nafasi ya kwanza wakiwa na Pointi 23.
Mchezo mwingine Azam FC wameichakaza Mtibwa Sugar mabao 4-3 mchezo uliopigwa uwanja wa Manungu Mkoa Morogoro.
Ligi hiyo itaendelea kesho katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza Kagera Sugar watawakaribisha Mabingwa watetezi Yanga ambao wapo nafasi ya tatu wakiwa na Pointi 20 huku wakiwa wanacheza mechi nane.
Leave a Reply
You must be logged in to post a comment.