Habari za michezo

HUYU MZAMIRU MPYA NI BALAA NA NUSU…KWA TAKWIMU ZAKE HIZI NDIO MAANA MGUNDA KAMGANDA…

admin November 12, 2022 6:36 pm

KIUNGO wa kazi ngumu ndani ya kikosi cha Simba, Mzamiru Yassin ni habari nyingine eneo la kati kutokana na kuimarika kwenye kila mchezo ambao ataanza.

Nyota huyo kwenye mchezo dhidi ya Singida Big Stars alikuwa na majukumu matatu, kupoka mipira kwa wapinzani, kulinda na kupeleka mashambulizi kwenye lango la wapinzani.

Asilimia 80 ya mipira aliyokuwa anapiga ilikuwa inafika kwa walengwa husika na kutokana na kazi ngumu aliyofanya alichezewa faulo dakika ya 19 na 37 na aliyeyusha dakika zote 90 bila kuonyeshwa kadi ya njano.

Kwenye ligi kacheza mechi 8 kayeyusha dakika 526, kafunga bao moja na katoa pasi moja ya bao msimu wa 2022/23 ni chaguo la kwanza la Kocha Mkuu wa Simba, Juma Mgunda.

YANGA WAIBUKA NA ‘MIHOGO PARTY’….ALLY KAMWE AFUNGUKA WANAOTAKIWA KUSHIRIKI… FT: SIMBA SC 1-0 IHEFU …SAKHO APIGA GOLI LA MSHINDO…AZAM FC WALITAMANI MECHI IISHE HARAKA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply