Habari za michezo

YANGA WAIBUKA NA ‘MIHOGO PARTY’….ALLY KAMWE AFUNGUKA WANAOTAKIWA KUSHIRIKI…

admin November 12, 2022 6:20 pm

OFISA Habari wa Yanga, Ally Kamwe amesema kuwa ushindi ambao wamepata ni zawadi kwa Wananchi na Tanzania kiujumla hivyo ni furaha kwa kila mtu.

Yanga metinga hatua ya makundi Kombe la Shirikisho Afrika kwa jumla ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Club Africain.

Mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Mkapa ubao ulisoma Yanga 0-0 Club Africain.

Bao la ushindi la Yanga lilifungwa na Aziz KI ambaye aliingia dakika ya 68 akitokea benchi alifunga dakika ya 79 kwa pasi ya Fiston Mayele.

Kamwe amesema:”Tumerejea kwenye ardhi ya Tanzania tukiwa na ushindi hii ni zawadi kwa kila Mtanzania na shabiki wa Yanga.

“Ambacho tunakifanya kwa sasa ni kuendelea kufurahi na tuna kazi ya ufanya Jumapili Mwanza ambapo kabla ya mchezo tutakuwa na party itakayoitwa,’Mihogo Party,’ mashabiki wajitokeze kwa wingi,” amesema.

Yanga ni namba moja kwenye msimamo ikiwa na pointi 20 baada ya kucheza mechi 8 za ligi.

UKIACHA CHAMA NA BANDA…HAWA HAPA MASTAA WENGINE SIMBA WATAKAOKOSEKANA LEO DHIDI YA IHEFU.. HUYU MZAMIRU MPYA NI BALAA NA NUSU…KWA TAKWIMU ZAKE HIZI NDIO MAANA MGUNDA KAMGANDA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply