Fei toto Yanga SC
Habari za michezo

BAADA YA KUONA AZAM HAWATANII KWA FEI TOTO…YANGA WAIONA ISIWE TABU…WAJA NA HILI …

admin November 17, 2022 6:08 am

Ikiwa imesalia takribani miezi miwili dirisha Dogo la usajili la mwezi Januari kufunguliwa, inasemekana Bosi wa Azam FC, Yusuf Bakhresa ameanza kufanya michakato ya kuboresha kikosi cha Azam na rada yake imetua kwa Nyota wa Yanga SC, Feisal Salum (Fei Toto).

Inasemekana Fei Toto na Bakhresa wapo mezani kujadili matakwa ya mchezaji huyo na endapo wataafikiana basi kiungo huyo aliyejizolea umaarufu mkubwa nchini akiwa na kikosi cha Yanga huenda akamwaga wino kuwatumikia matajiri wa Jiji la Dar es Salaam.

Fei Toto ana Mkataba na mabingwa hao watetezi hadi mwaka 2024 na inasemeka kuwa kuvunja mkataba wake anahitajika kuwalipa Yanga Tsh. milioni 100 na mshahara wake wa miezi mitatu.

Klabu ya Yanga SC imeeleza kuwa, watu waache kuota, Feisal Salum hauzwi kwa gharama yoyote.

Msemaji wa klabu hiyo Alli Kamwe alipoulizwa kuhusu tetesi zilizozagaa leo zikianzishwa na kituo cha Wasafi FM kuwa Azam FC imeandaa kitita ili kumnunua Feisal dirisha dogo, Alli Kamwe amesema;

“Feisal kwenda Azam ?! Labda atakwenda kwenye boti ya AZAM MARINE wakati akielekea nyumbani kwao Zanzibar. Hakuna klabu inayoweza kumnunua Feisal Salum kutoka Yanga hapa Tanzania labda nje,” amesema Ally Kamwe.

IMEFICHUKAAA…TATIZO SIO MGUNDA…NABI AWACHANA MASTAA YANGA..AWAPA SIKU TISINI ZA MOTO… RASM…KISA YACOUBA…AIDHA KISINDA AU MAKAMBO MMOJA LAZIMA ASEPE YANGA..ISHU IKO HIVI…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

One response to “BAADA YA KUONA AZAM HAWATANII KWA FEI TOTO…YANGA WAIONA ISIWE TABU…WAJA NA HILI …”

  1. Harun Msemwa says:

    Mpira ni biashara for real sijaona kwa kuuchezea feisal hapa bongo zaidi ya young Africans

Leave a Reply