Mzamiru akiwajibika Simba SC
Habari za michezo

MANDLA: WATU WANACHUKULIA POA TU…SIMBA TIMU KUBWA AFRIKA..

admin November 18, 2022 8:27 pm

Kocha mpya wa Viungo Simba SC Kelvin Mandla amefunguka kwa mara ya Kwanza baada ya kutambulishwa rasmi na Uongozi wa Klabu hiyo jana Alhamis (Novemba 17).

Mandla ametambulishwa Klabuni hapo akichukua nafasi ya Kocha Sbai Karim aliyeoondoka na Kocha Mkuu Mserbia Ziran Maki mapema mwezi Septemba mwaka huu.

Kocha Mandla amesema amefurahi kujiunga na Klabu ya Simba SC ambayo imekua na muendelezo mzuri katika Michuano ya Afrika, huku akiahidi kujitoa kwa moyo wake wote ili kuiwezesha kupata mafanikio msimu huu 2022/23.

“Simba ni timu kubwa, ni timu ambayo sio tu inashiriki bali kushindana kwenye michuano ya CAF. Nitazamia kuungana nao katika jambo hilo na kusaidia timu kwenda mbele zaidi ya ambapo imewahi kufika,” amesema Mandla alipohojiwa kupitia Simba TV.

Kabla ya kutambulishwa kwa Kocha Mandla, Simba SC ilimtambulisha Kocha wa Makipa Chlouha Zakaria mwanoni mwa juma hili.

KAGERE: KWA YANGA HII…UBINGWA NI WAO TENA…WAMEKAMILIKA KILA IDARA… PAMOJA NA KUIPELEKA YANGA MAKUNDI CAF…NABI APATA WENGE NA KIKOSI CHAKE..

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply