Habari za michezo
MCHEZO WA DAKIKA ZA KUSIMAMA WARUDI TENA YANGA…LEO ZAMU YA GSM…
admin
November 22, 2022
1:21 pm
Leo Jumanne, Novemba 22, 2022, Yanga itashuka uwanja wa Liti mkoani Singida kuikabili Dodona Jiji kwenye mchezo wa ligi kuu ya NBC.
Afisa habari wa Yanga Ally Kamwe amesema kesho katika mchezo huo watafanya matukio mawili makubwa.
Kwanza ni kuendeleza utaratibu wa kuwapongeza wachezaji na benchi la ufundi baada ya kucheza mechi 47 za ligi kuu bila kupoteza.
Tukio hilo litafanyika katika dakika 47 ya mchezo ambapo mashabiki wa Yanga watasimama kwa dakika moja kuwapigia makofi wachezaji pamoja na benchi la ufundi.
Lakini pia tukio hilo litakwenda sambamba na pongezi kwa Mfadhili/Mdhamin wa klabu ya Yanga Ghalib Said Mohammed ‘GSM’ ambaye juzi ilikuwa siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwake.
Wananchi watatumia mechi dhidi ya Dodoma Jiji kumshukuru na kumtakia kila la kheri katika majukumu yake
GSM ndiye chachu ya furaha ya Wananchi kwa sasa, uwekezaji wake ndani ya klabu ya Yanga umekuja na mafanikio makubwa.
Leave a Reply
You must be logged in to post a comment.