Habari za michezo

KISA SARE NA MBEYA CITY….MGUNDA KAONA ISIWE SHIDA…KAAMUA KUWATUPIA LAWAMA MABEKI…

admin November 25, 2022 6:00 am

Kocha Mkuu Juma Mgunda, ameweka wazi kuwa kutoka sare ni sehemu ya mpira na hawezi kumtupia lawama mchezaji mmoja mmoja.

Mgunda amekiri kuwa safu  ya ulinzi ilishindwa kutimiza majukumu yake vizuri na kuruhusu Mbeya City kupata bao rahisi la kusawazisha lakini ndiyo sehemu ya mpira huwezi kufanya kila kitu kwa usahihi ndani ya dakika 90.

Mgunda ameongeza kuwa hakuna mchezaji ambaye anapenda kufungisha ili timu yake kupoteza au kupata sare kinachotokea ni sehemu ya mchezo.

“Kwanza lazima tukubaliane kutoa sare kwenye mpira si dhambi, niwapongeze Mbeya City kwa kucheza vizuri na kutumia udhaifu wetu kupata bao la kusawazisha, sisi tunarudi mazoezini kujiandaa na mchezo unaofuata.

“Matokeo haya bado hayajatukatisha tamaa tutaendelea kupambana hadi mwisho kupigania ubingwa,” amesema Mgunda.

DAKTARI AFICHUA KILICHOMKUMBA MWAMNYETO JUZI…ALIKUWA AHEMI TENA… WAKATI SIMBA WAKILIA NA AINA YA WACHEZAJI WAO…NABI KAFUNGUKA HAYA KUHUSU MASTAA WAKE YANGA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply