Habari za Yanga
Habari za michezo

WAKATI SIMBA WAKILIA NA AINA YA WACHEZAJI WAO…NABI KAFUNGUKA HAYA KUHUSU MASTAA WAKE YANGA…

admin November 25, 2022 6:03 am

KOCHA Nasreddine Nabi amesema anajivunia sana wachezaji wa kikosi chake cha Yanga kutokana na upambanaji wao waliouonyesha kwenye mchezo dhidi ya Dodoma Jiji FC.

Mchezo huo uliopigwa kwenye dimba la CCM Liti mkoani Singida ulimalizika kwa Wananchi kubeba alama tatu baada ya ushindi wa mabao 2-0.

Akizungumza baada ya mchezo huo, Nabi amesema walikutana na timu ngumu sana lakini wachezaji wake walijituma mno kuhakikisha wanaondoka na ushindi.

“Dodoma ni timu ngumu inayocheza soka la nguvu sana. Walitupa wakati mgumu na wachezaji wangu walikuwa bado na mchoko wa safari.

“Lakini unaweza kuona namna vijana walivyojitoa na kupambana kuhakikisha tunashinda mchezo huu. Najivunia sana wachezaji wangu na huu ni ushindi wa zawadi kwa mashabiki wetu,” alisema Nabi.

KISA SARE NA MBEYA CITY….MGUNDA KAONA ISIWE SHIDA…KAAMUA KUWATUPIA LAWAMA MABEKI… KITENDO CHA KUIFUNGA ARGENTINA TU…SAUDI ARABIA WAMEVUNJA NA KUWEKA REKODI HIZI KIBAO…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply