Home Habari za michezo BAADA YA KUONA MAMBO MAGUMU…YANGA WAAZIMA WACHEZAJI SIMBA ILI WAFUZU CAF…

BAADA YA KUONA MAMBO MAGUMU…YANGA WAAZIMA WACHEZAJI SIMBA ILI WAFUZU CAF…

Mabingwa wa mara nyingi zaidi wa Tanzania, Yanga SC jioni ya leo watashuka kwenye dimba la Benjamin Mkapa kuliwakilisha taifa kwa mara nyingine tena kwenye mchezo wa mtoano wa kombe la Shirikisho barani Afrika ‘play off’ hatua ya kwanza, baada ya kuondoshwa kwenye mashindano ya klabu bingwa (CAFCL).

Yanga watacheza mchezo wao majira ya saa 10:00 jioni, dhidi ya miamba kutoka Tunisia Club Africain, ambapo Yanga itahitaji kushinda mchezo wa leo ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kufuzu hatua ya makundi kabla ya mchezo wa marudiano utakaopigwa nchini Tunisia.

Leo nataka nikurudishe nyuma miaka 24 iliyopita ikiwa ndiyo mara ya mwisho kwa Yanga kufuzu hatua ya makundi CAFCL, ilikuwa ni mwaka ambao Yanga ilifanikiwa kutinga hatua ya makundi CAF na kuwa klabu ya kwanza Afrika Mashariki kutinga makundi.

Yanga Waliishia kupewa jina la “Jamvi la Wageni” kwa maana game yao ya kwanza tu dhidi ya Raja Casablanca walikutana na kipigo cha ‘kikubwa baada ya kuchapwa 6-0, wakapigwa 3-0 na Asec Mimosa katika uwanja wa Uhuru, wakaenda Afrika Kusini wakapigwa 4-0 na Manning Rangers.

Kutokana na mambo kuwa magumu, Yanga wakawaazima wachezaji watatu watani zao Simba SC ambao ni Monja Liseki,Shabani Ramadhani na Alphonce Modest wakawasaidie mchezo dhidi ya Asec Mimosas.

Yanga iliwachezesha wachezaji wote walioazimwa na Simba na kusaidia kupunguza idadi ya magoli Walipoteza ugenini 2-1 dhidi ya Asec Mimosa Matokeo 1-1 dhidi ya Manning na 3-3 dhidi ya Raja Casablanca katika uwanja wa Uhuru yalikuwa mazuri zaidi kwao katika michezo 6 ambayo walimaliza wakiwa wameruhusu magoli 19 na kufunga magoli matano tu.

Kipindi hicho Simba na Yanga hawakuwa na Uadui kama huu wa zama hizi, walikuwa ni watani tu wa jadi kwenye mambo ya kutetea taifa walikuwa ni wamoja, ni wakati sasa wa kuungana kwa timu hizi za Simba na Yanga.

SOMA NA HII  TAZAMA PICHA MUKOKO AKIWA MAZOEZINI MOROCCO NA TIMU YAKE YA YANGA