Home Habari za michezo BAADA YA KUONA MECHI NA WATUNISIA LEO NI NGUMU…NABI KAONA ISIWE TABU…AITAJA...

BAADA YA KUONA MECHI NA WATUNISIA LEO NI NGUMU…NABI KAONA ISIWE TABU…AITAJA SIMBA…

Habari za Yanga SC

Yanga leo itakuwa uwanja wa Mkapa kuwakabili Watunisia katika mechi ya mtoano kuwania kufuzu hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika, lakini kocha Nasreddine Nabi amesema ana kazi kubwa ya kuhakikisha washambuliaji wake wanatumia vyema nafasi za kufunga ili kuimaliza mechi nyumbani.

Yanga leo Jumatano itaikaribisha Club Africain ya Tunisia kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam na marudiano ya mchezo huo yatafanyika wiki ijayo, huku timu itakayofuzu itaingia katika hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho inayoanza kuchezwa Februari mwakani.

Nabi alisema maandalizi ya mchezo huo yalianza mapema mara baada ya kucheza mechi ya dabi dhidi ya Simba kwani alitenga muda wa kutosha kuwaangalia wapinzani wao namna mbinu zao zilivyo inapokuwa ugenini.

Alisema sasa sio muda wa kufanya mazoezi magumu ila wanafuatilia zaidi mbinu na mambo ya kiufundi ambayo wameyaona na kuyafanyia kazi ili kuhakikisha wanapata ushindi mkubwa nyumbani.

“Ligi ya Mabingwa Afrika tulishindwa kufanya vizuri kutokana na kukosa matokeo bora nyumbani safari hii tumejipanga kuhakikisha tunapata matokeo bora katika mchezo huu wa kwanza ili tukamalize kazi ugenini,” alisema Nabi na kuongeza;

“Baada ya kucheza na Simba tulipumzisha baadhi ya wachezaji wa kikosi cha kwanza kwenye michezo miwili iliyofuata dhidi ya KMC na Geita Gold ndio maana kuna wakati tulishindwa kucheza kwa ubora,

“Tuliwapumzisha wachezaji hao ili miili yao iondoe uchovu na siku ya mchezo na Club African iwe freshi zaidi kwa ajili ya kupambana, tofauti kama wangetumika kwenye michezo miwili iliyofuata baada ya kucheza na Simba.

“Kuna kazi kubwa inahitajika kufanyika kwa wachezaji wangu ili kupata ushindi mkubwa na hilo litawezekana kutokana na maelekezo ya kiufundi niliyowapatia pamoja na kile tulichokiona kutoka kwa wapinzani.

“Malengo yetu ni kwenda hatua ya makundi na hilo naamini linawezekana kutokana na hamu kubwa iliyopo kwa wachezaji wangu.” alisema Nabi ambaye katika mechi zilizopita za Ligi, aliwapumzisha nyota wake na wengine wakianzia benchini ambao ni Fiston Mayele, Djuma Shabani, Yannick Bangala, Aziz Ki, Feisal Salum na Tuisila Kisinda. Soma uchambuzi wa mtoto wa Nabi ukurasa wa 12.

SOMA NA HII  HUU HAPA UKWELI KUHUSU ''MAHUSIANO YA KI...ZI..'' KATI YA MANARA NA MWAMNYETO