Home Habari za michezo BAADA YA MZUNGUKO WA KWANZA KUISHA…KIKOSI BORA CHA MASTAA WA NNJE HIKI...

BAADA YA MZUNGUKO WA KWANZA KUISHA…KIKOSI BORA CHA MASTAA WA NNJE HIKI HAPA…

Mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Tanzania Bara umekamilika juzi Disemba 7 kwa michezo miwili ambapo Yanga wamemaliza kibabe wakiichapa Namungo huku Coastal wakiiduwaza Singida kwa kipigo cha magoli 2-1.

Wapo mastaa ambao wamefanya mambo mazito katika mzunguko huu ambao mpaka makala hii inatengenezwa vinara wa msimamo wa Ligi Kuu Bara walikuwa Yanga pale juu na wafuatao ni mastaa wa kigeni ambao wanaunda kikosi cha kwanza kwa wachezaji wa kigeni kulingana na takwimu zao viwanjani

Djigui Diarra

Kipa namba moja wa Yanga ambaye mpinzani wake ni mzawa yule wa Simba, Aishi Manula, Diara msimu huu ameshacheza mechi 11 mpaka sasa sawa na dakika 990 uwanjani. Takwimu zake bora zingine ni kuwa na sevu 13 pia akiokoa penalti 1.

Nicholas Gyan

Akiwa na klabu yake ya Singida Big Stars amekuwa akitumika kama beki wa kulia na hata winga wa kulia. Mpaka sasa amefanikiwa kutengeneza asisti 4 kwenye ligi akimzidi beki mwingine wa kulia Nicholas Wadada wa Ihefu aliyetengeneza asisti moja na bao 1 katika michezo 9 aliyocheza sawa na dakika 772.

Bruce Kangwa

Beki wa kushoto wa Azam ataendelea na jukumu hilo kwenye kikosi hiki kutokana na kazi bora yake Azam Complex, akicheza michezo 10, sawa na dakika 810 ingawa hana bao wala asisti.

Henock Inonga

Beki wa kati wa Simba ambaye ameendelea na kuwa na wakati mzuri katika michezo 14 aliyocheza sawa na dakika 1260 akikosa mechi moja tu baada ya kuugua kabla ya mchezo kuanza.

Joash Onyango

Kando na Inonga mtu ambaye anamuongezea ubora Mkongomani huyo ni Mkenya huyu ambaye msimu huu alirejea na nguvu akiutihibitishia uma wa klabu yake kwamba bado anastahili kuvaa jezi za wekundu hao akicheza michezo 12 sawa na dakika 990.

Khalid Aucho

Kiungo mkabaji wa Yanga ambaye amekuwa mhimili mkubwa kwa timu yake ndani ya miaka miwili hii, msimu huu amecheza michezo 12 sawa na dakika 812 alizokuwa uwanjani lakini ukiacha ukabaji wake pia ametoa asisti 2.

Yannick Bangala

Pembeni ya Aucho mashabiki wa Yanga wanafurahia kupenda kumuona huyu ambaye alikuwa mchezaji bora wa msimu uliopita, akicheza mechi 11 sawa na dakika 911 akiwa na bao moja tayari.

James Akamiko

Kiungo fundi wa Azam anayecheza msimu wa kwanza hapa nchini lakini akianza katika kiwango bora, akicheza michezo 13 sawa na dakika 950 akiwa na bao 1 na asisti 2

Fiston Mayele

Mshambuliaji wa Yanga anayeongoza kwa ufungaji katika ligi akiwa amefunga mabao 10 akiwa na asisti 1 akicheza michezo 12 sawa na dakika 897.

Mosses Phiri

Pembeni ya Mayele atacheza mshambuliaji huyu wa Simba ambaye ameendelea kuwa na moto katika msimu wake wa kwanza hapa nchini naye akifunga mabao 10, akimzidi asisti moja Mkongomani huyo katika michezo 15 aliyocheza sawa na dakika 1275.

Clatous Chama

Kiungo fundi wa Simba huyu ambaye amekuwa na moto mkali msimu huu na hakuna aliye bora kwa wageni kwa nafasi yake kumzidi mkapa sasa akicheza michezo 12 sawa na dakika 1057 akikosa mechi tatu kutokana na kusimamishwa michezo 3, akifunga mabao 2 huku akitoa asisti 7, akimzidi Ayoub Lyanga kwa asisti moja pekee.

Sub

Kwenye wachezaji wa akiba kanuni inataka timu kuwa na wachezaji wasiopungua 7 ambapo mastaa hawa wanaweza kuwa hapa wakisubiri kucheza katika kikosi cha kwanza.

Arakaza MC Artur,

Nico Wadada,

Biemes Carno,

Moubarack Amza,

Jesus Moloko,

Idris Mbombo na

Sadio Kanoute

KOCHA NASREDDINE NABI

Kocha huyu wa Yanga atakuwa na kikosi hiki achana na kutofungwa mechi 49, lakini msimu huu amepoteza mechi moja iliyositisha rekodi hiyo ngumu na pia akiwa tayari na tuzo moja ya kocha bora huku pia timu yake ikiongoza ligi.

SOMA NA HII  KISA VITA VYA WACHAMBUZI NA AZIZI KI....ALLY KAMWE AFUNGUKA HAYA YA MOYONI...