Tetesi za Usajili Bongo
Habari za michezo

TETESI ZA USAJILI: BAADA YA KUONA MAMBO NI MAGUMU YANGA…MAKAMBO KUMFUATA ZAHERA….

admin December 12, 2022 11:00 am

Kikosi cha Polisi Tanzania kimekuwa na msimu mbaya hadi sasa kikiburuza mkia katika msimamo wa Ligi Kuu, kikikusanya pointi tisa tu katika mechi 15, lakini mabosi wa klabu hiyo hawajalala kwani wamempa timu Mwinyi Zahera na kocha huyo fasta amemchomoa straika mmoja kutoka Yanga.

Zahera aliyewahi kuinoa Yanga, ametua Polisi kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Joslin Bipfubusa aliyetemwa hivi karibuni na katika moja ya kazi aliyopewa ni kuleta majembe ya kuinusuru timu hiyo kwenye duru la pili na tayari ameshapendekeza jina moja ambalo ni la Heritier Makambo wa Yanga.

Makambo kwa sasa yupo kwao DR Congo alipoenda kwa matatizo ya kifamilia, lakini tayari yupo kwenye rada za Zahera aliyemsajili wakati akiwa Yanga kabla ya kuuzwa AC Horoya ya Guinea na kurejea msimu huu Jangwani, timu ikinolewa na Nasreddine Nabi.

Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya uongozi wa Polisi, kimeliambia Mwanaspoti, kuwa wamefanya makubaliano na mabosi wa Yanga ili wawaachie mshambuliaji huyo, aliyemaliza na mabao 17 msimu wa 2018-2019 nyuma ya Meddie Kagere aliyekuwa na Simba na Salim Aiyee aliyekuwa Mwadui.

Makambo alijiunga na Yanga kwa mkataba wa miaka miwili msimu uliopita akitokea Horoya lakini hajawa na makali kiasi cha kukosa namba mbele ya Fiston Mayele katika kikosi cha kwanza na Zahera aliyekuwa mkurugenzi wa soka la Vijana Yanga amewakodeza Polisi kuwa yeye anamjulia straika huyo.

Inaelezwa Zahera amewahakikisha Polisi wakimchukua Makambo akaungana na kina Vitalis Mayanga na wenzao waliopo kikosini atafanya makubwa kwani anajua namna ya kumtumia kama alivyofanya alipokuwa naye Yanga na kufunga mabao ya kutosha katika msimu wa kwanza tu Jangwani.

“Mazungumzo na uongozi wa Yanga yanakwenda vizuri tunatarajia mchezaji ataweza kukubaliana na ofa yetu kutokana na Zahera kuongeza nguvu kwenye mchakato huo,” kilisema chanzo hicho ambacho hakikutaka jina lake litajwe, kichoongeza:

“Mbali na usajili huo kama utakamilika bado tutaongeza kiungo mkabaji na mshambuliaji na safu ya ulinzi itaongezewa nguvu lengo ni kuunda kikosi kitakachotoa ushindani katika duru la pili na kuisaidia timu iweze kubaki Ligi Kuu.”

TETESI ZA USAJILI:..YANGA WAIZIDI KETE SIMBA KWA BOBOSI..ASAINISHWA KININJA …ISHU NZIMA IMEFANYIKA DUBAI… HUYU HAPA DOGO MTZ ALIYEPATA SHAVU LA KUCHEZA LIGI MOJA NA MESSI WA PSG…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply