Home Habari za michezo ACHANA NA STORI MBAO….MANZOKI ANAKUJA NA MAMBO HAYA MATATU SIMBA…

ACHANA NA STORI MBAO….MANZOKI ANAKUJA NA MAMBO HAYA MATATU SIMBA…

Wakati Klabu ya Simba ikielekea kwenye uchaguzi mkuu Januari 29, 2023, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba, Salim Abdallah ‘Try again’ ameibuka na kutaja mambo matatu muhimu klabuni hapo ikiwemo usajili wa mshambuliaji wa Dalian Professional ya China, Cesar Manzoki.

Mwanzoni mwa msimu huu, iliripotiwa kwamba, Manzoki amemalizana na Simba kwa ajili ya kuichezea timu hiyo, lakini usajili wake uliingia doa kutokana na timu yake ya awali ya Vipers kuweka ngumu, hali iliyowafanya kumpeleka China kujiunga na Dalian Professional ambapo mkataba wake unamalizika Desemba 31, mwaka huu.

Try Again ametoa ufafanuzi wa mambo hayo matatu ikiwemo usajili watakaoufanya katika dirisha dogo kuelekea hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Kiongozi huyo wakati akifafanua mambo hayo kupitia akaunti yake ya Twitter, aliambatanisha na picha ambayo ina watu watatu, lakini haioneshi vichwa vyao.

Uchunguzi uliofanywa  kuhusu picha hiyo, imebainika kwamba miongoni mwao ni Manzoki akiwa katikati kutokana na michoro yake ya mkononi ‘Tatoo’ kuonekana.

Try Again alibainisha kwamba: “Wanasimba katika kipindi hiki ‘focus’ yetu ni kuimarisha benchi la ufundi liwe bora zaidi, kufanya usajili bora na sahihi, na wa nguvu ili kuiboresha timu yetu iweze kuwa tayari kupambana kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika na pia kuendelea kupambana kwenye ligi kuu ili tuchukue ubingwa.

“Kufanya uchaguzi huru na wa haki ili kupata viongozi bora wa kuiongoza klabu yetu. Naomba wapenzi na wanachama tupuuze porojo za wasioitakia mema klabu yetu. Simba ni imara na salama na itabaki kuwa hivyo daima. Simba NguvuMoja.”

Kauli ya Try Again, inakuja siku chache baada ya Mtendaji Mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez kutangaza kujiuzulu nafasi yake hiyo aliyodumu kwa takribani miaka miwili.

Ikumbukwe kuwa, Simba ambayo inapambana kuboresha kikosi chao, pia ipo kwenye mchakato wa kusaka kocha wa kusaidiana na Juma Mgunda ambaye alikabidhiwa kikosi hicho alipoondoka Zoran Maki, Septemba, mwaka huu.

SOMA NA HII  BAADA YA KUONA SIMBA HAWATANII...YANGA WAMUAMULIA JOB...MKTABA WAKE MPYA NI KUFRU TUPU...