Habari za michezo

KISA KUNYIMWA PENATI JUZI…MOROCCO WAPANGA KUKIMBILIA MAHAKAMANI KUDAI HAKI YAO…

admin December 16, 2022 10:48 am

Shirikisho la Soka la Morocco (FRMF) limetangaza Alhamisi, Desemba 15, kwamba limewasilisha malalamiko yake kwa ‘chombo chenye uwezo’ (bila kutaja jina) kupinga usimamizi wa mechi ya nusu fainali ya michuano ya Kombe la Dunia 2022, ambapo Simba wa Atlas walifungwa na Ufaransa 2-0 siku ya Jumatano.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, FRMF inarejea kwenye maamuzi mawili ya ussimamizi wa mechi “baada ya kuinyima Morocco penalti mbili zisizopingika kwa maoni ya wataalamu kadhaa”.

Shirikisho la soka la Morocco linazungumzia kitendo kilichotokea katika dakika ya 27 wakati Sofiane Boufal na Théo Hernandez walipokutana katika eneo hilo, na ambapo mwamuzi kutoka Mexico, César Arturo Ramos, alitoa onyo kwa Morocco.

Shirikisho hilo pia limekosoa kutopigwa kwa penalti ambayo mwamuzi alikubali mwenyewe, kabla ya mapumziko, wakati Youssef En-Nesyri alijikuta amedondoshwa baada ya kugongana na Aurélien Tchouaméni. FRMF inashangaa kwamba mwamuzi kupitia video “haikujibu hali hizi”. Rufaa yake kwa hakika haina nafasi ya kushinda.

BAADA YA KUONA WAMEPANGWA NA WAARABU ….PHIRI AIBUKA NA HILI KUHUSU HATMA YA SIMBA CAF.. TETESI….THOMAS ULIMWENGU NI  SIMBA AU YANGA…DILI LAKE LIKO HIVI…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply