Geita Gold FC

FT:GEITA GOLD 0 – 5 SIMBA SC…..KIBU DENIS AMPIGA BUSU CHAMA…SAKHO KAMA MESSI VILEE…

admin December 18, 2022 6:54 pm

Klabu ya Simba imefanikiwa kuondoka pointi tatu na kufanikisha kufunga mabao 5-0 dhidi ya timu ya Geita Gold, mchezo ambao ulipigwa kwenye dimba la CCM Kirumba Jijini Mwanza.

Simba Sc katika mchezo huo aliweza kutawala mchezo kuanzia katikati ambako kulisaidia kuzalisha mabao hayo ya aina yake.

Simba Sc kwenye kipindi cha kwanza walicheza kwa kushambulia na kufanikiwa kupata mabao ya haraka kupitia kwa mshambuliaji wao John Bocco akifungwa kwa kichwa huku goli la pili likifungwa na Chama.

Katika kipindi cha pili Simba ilirudi ikiwa inahitaji mabao mengi kwani imekuwa ikishambulia kwa kasi ndipo ikafanikiwa kupata mabao mengine matatu kupitia kwa nyota wao Sakho aliyefunga mawili na goli la mwisho amefunga Kibu Dennis ambaye aliingia kipindi cha pili.

Baada ya kufunga goli hilo, ambalo ni goli lake la kwanza kwa msimu huu, Kibu Denis alimfuata Chama na kumbusu kwenye miguu yake kama ishara ya kukubali kile alichokifanya, haswa ukizingatia kuwa pasi ya goli hilo ilitoka kwa Chama.

BAADA YA KUSIKIA AZAM NA SINGIDA ZINAMFUKUZIA SAIDO…SIMBA NAO WAJIBU MAPIGO KIBABE…ISHU YOTE IKO HIVI… ACHANA NA STORY ZA VIJIWENI…ILE ISHU YA JOB KUTAKIWA MISRI..UKWELI WOTE HUU HAPA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply