Home Habari za michezo ALICHOSEMA MGUNDA BAADA YA ‘KUITIFUA’ GEITA GOLI 5….KAGERA SUGAR KAZI MNAYO AISEE….

ALICHOSEMA MGUNDA BAADA YA ‘KUITIFUA’ GEITA GOLI 5….KAGERA SUGAR KAZI MNAYO AISEE….

Kocha Msaidizi Simba, Juma Mgunda

Licha ya kufanikiwa kuibuka na ushindi mnono wa mabao 5-0 kocha Juma Mgunda ameisifu Geita Gold na kusema ni timu nzuri na imewapa ushindani mkubwa.

Mgunda amesema mpira ni mchezo wa makosa ambapo Geita Gold waliyofanya na wao kukayatumia vizuri kupata ushindi mnono.

Mgunda ameongeza kuwa tangu wanatoka Dar es Salaam kwenda Mwanza walikuwa wanajua wanaenda kukutana na timu imara na walijipanga kuwakabili.

โ€œKupata ushindi mabao matano haimaanishi Geita ni timu mbovu, bali mpira ni mchezo wa makosa wameyafanya tumeyatumia vizuri.

โ€œJambo jema tumepata alama tatu ugenini tunajipanga kwa mchezo ujao wa ligi dhidi ya Kagera Sugar,โ€ amesema Mgunda.

SOMA NA HII  SIMBA YAMKUMBUKA BALEKE...REKODI YAKE HII HAIJAVUNJWA HADI LEO...SIKU 125 ZATIMIA