Azam FC

FT: AZAM FC 2-3 YANGA SC…….SOPU AMSOPOA DIARRA MAR TANO…

admin December 25, 2022 10:31 pm

WAKICHEZA bila kiungo wao Fei Toto timu ya Yanga SC imeichapa Azam FC mabao 3-2 mchezo wa Ligi Kuu ya NBC uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar Es Salaam.

Azam FC walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa Abdul Sopu dakika ya 27 akimalizia pasi ya Prince Dube huku Yanga wakipata mabao kupitia kwa Fiston Mayele dakika ya 31 na Stephane Aziz Ki dakika ya 33 na kuenda mapumziko Yanga wakiwa wanaongoza.

Kipindi cha pili Azam FC walipata bao la mapema dakika ya 47 likifungwa na Abdul Sopu ambalo ni goli lake la 5 dhidi ya Diarra na bao la ushindi la Yanga SC likifungwa na Farid Mussa dakika ya 78.

Kwa ushindi huo Yanga SC wamefikisha Pointi 47 na kuiacha Azam FC kwa tofauti ya Pointi 10 huku wakicheza bila kiungo wao Fei Toto anayedaiwa kusajiliwa na Azam FC.

NABI AGOMA KISA FEI TOTO….ATOA MAELEZO HAYA KWA MASTAA YANGA SC.. JEURI YA PESA YANGA SC….MTOGO ASHUSHWA BONGO CHAP…STRAIKA MGHANA HUYOOO SIMBA SC…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply