Habari za Simba
Habari za michezo

NTIBAZONKIZA AANZA NA MGUU WA KULIA SIMBA SC…’AKICHAFUA ILE ILE’ MAZOEZINI…

admin December 25, 2022 8:11 pm

Hatimaye kwa mara ya kwanza kiungo mshambualiaji wa Simba SC Saido Ntibazonkiza leo amejumuika na wachezaji wenzake kwenye mazoezi ya jioni ikiwa ni siku moja toka atangazwe.

Saido ambaye niusajili mpya na wa kwanza kwa Simba SC toka kufunguliwa kwa dirisha doho la usajili tarehe 15 mwezi huu, amejiunga na timu hiyo ambayo iko Mwanza ikijiandaa kucheza mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya KMC hapo kesho.

Zifuatazo ni sehemu ya picha za tukio hilo, ambapo zinamuonyesha Saido akiwa na furaha kujiunga na Simba SC akiwa ni sehemu ya wachezaji wachache wa kigeni ambao wamepata nafasi ya kucheza Simba na Yanga .

Saido Ntibazonkiza akisalimiana na Kibu Denis leo kwenye mazoezi ya Simba SC

Saido Ntibazonkiza akionyesha ufundi mbele ya Kaimu Kocha Mkuu wa Simba SC, Juma Mgunda

Kulingana na mazoezi ya leo, huenda kesho Kaimu Kocha MKuu wa Simba , Juma Mgunda akashawishika kumuanzisha katika kuhakikisha wanapata ushindi dhidi ya KMC.

Saido Ntibazonkiza akipokea maelekezo ya kiufundi kutoka kwa Kaimu Kocha Mkuu wa Simba SC, Juma Mgunda

Saido Ntibazonkiza amejiunga na SimbaΒ  akitokea Geita Gold FC kwa mkataba wa mwaka mmoja na nusu,awali mchezaji huyo ambaye pia ni Nahodha wa timu ya Taifa ya Burundi aliwahi pia kuichezea YangaΒ  kabla ya kutemwa kwa kile kilichosemekana kuwa ni ukosefu wa nidhamu.

WAKATI FEI TOTO AKIIKACHA TIMU HUKU MAYELE AKISEPA KWAO….YANGA SC WAMPA ‘MZIGO’ AZIZ KI… NABI AGOMA KISA FEI TOTO….ATOA MAELEZO HAYA KWA MASTAA YANGA SC..

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply