Azizi Ki akiwajibika Yanga SC
Habari za michezo

WAKATI FEI TOTO AKIIKACHA TIMU HUKU MAYELE AKISEPA KWAO….YANGA SC WAMPA ‘MZIGO’ AZIZ KI…

admin December 25, 2022 7:46 pm

Kocha Mkuu wa Yanga SC, Nasreddine Nabi amependekeza majina ya mastaa saba kupewa muda wa mapumziko kutokana na kutumika zaidi, huku akisisitiza Stephen Aziz Ki ndiye atakayeiongoza timu hiyo kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi 2023.

Yanga SC inatarajia kuanza mechi ya kwanza ya Mapinduzi dhidi ya KMKM siku ya Januari 4 mwakani. Nabi amemtaja Fiston Mayele, Yanick Bangala, Khalid Aucho, Dickson Job, Kibwana Shomari, Jesus Moloko na Feisal Salum ‘Fei Toto’ kuwa ni wachezaji ambao wametumika zaidi hadi sasa hivyo wanatakiwa kupumzishwa kwaajili ya kuiweka miili sawa.

Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya timu hiyo kimesema wachezaji hao hawatakuwa miongoni mwa mastaa watakaocheza mechi ya kwanza ya Mapinduzi kutokana na nafasi ya mapumziko waliyopewa na kocha.

“Mfano Mayele akimaliza mechi na Mtibwa Sugar atakuwa na safari ya kwenda Congo kwaajili ya kufuatilia hati yake ya usafiri (pasipoti) ambayo imeshakwisha muda wake na Yanga ina mashindano ya kimataifa,” kilisema chanzo hicho na kuongeza;

SIMBA SC HAWATANII AISEE…BAADA YA MRENO KUCHOMOA…KOCHA MPYA HUYU HAPA… NTIBAZONKIZA AANZA NA MGUU WA KULIA SIMBA SC…’AKICHAFUA ILE ILE’ MAZOEZINI…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply