Habari za michezo

FT: KMC 1 – 3 SIMBA SC…..BOCCO AANZA KURUDI…NTIBAZOKINZA APIGWA JUKWANI…

admin December 26, 2022 6:21 pm

KLABU ya Simba SC imefanikiwa kuondoka na alama tatu mbele ya timu ya KMC FC kwa kuishushia kipigo cha mabao 3-1, mchezo ambao ulipigwa kwenye dimba la CCM Kirumba Jijini Mwanza.

Simba sC ilianza kupata bao kipindi cha kwanza kupitia kwa nahodha wao, John Bocco na kuwatanguliza mbele mpaka mapumziko wakiwa mbele kwa 1-0 kabla ya KMC kusawazisha.

Simba SC ilipata bao la pili kupitia kwa nyota wao Okra na baadae beki wao kisiki raia wa DR Congo, Henock Inonga akifunga mahesabu kwenye mchezo huo na kufanya matokeo kuwa 3-1.

Aidha katika mchezo huo, Kiungo Mshambuliaji mpya wa Simba , Saido Ntibazonkiza ameshindwa kupangwa kuwemo kwenye kikosi kilichoanza kwa kile kilichosemekana kuwa bado hajawa fiti kuingia kwenye kikosi cha Simba moja kwa moja.

Kiungo huyo alikuwa jukwani sambamba na wachezaji wengine wa Simba, hivyo huenda akajumuishwa kwenye mechi zijazo.

FEI TOTO AENDELEA ‘KUIDELETE’ YANGA SC KIAINA…AKATAA KUTAMBULIKA KAMA MCHEZAJI WAO… MKATABA WA SAIDO NA SIMBA SC KUFURU TUPU…NABI AWAKA YANGA SC….MAKAMBO ATUPIWA VIRAGO…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply