Chama na Simba SC Msimu Huu
Habari za michezo

BALAA LA CHAMA NDANI YA SIMBA SC MSIMUU SIO KITOTO…TAKWIMU HIZI HAPA…

admin December 27, 2022 11:18 am

KINARA wa pasi za mwisho ndani ya Ligi Kuu Tanzania Bara na Simba SC, Clatous Chama ana hatari kila baada ya dakika 104 akiwa uwanjani.

Ni mabao matatu katupia kibindoni akiwa ametoa jumla ya pasi 9 anafuatiwa na Ayoub Lyanga wa Azam FC ambaye ametoa pasi 7 na katupia bao moja.

Simba SC ikiwa imetupia mabao 37 baada ya kucheza mechi 17, nyota huyo kahusika kwenye jumla ya mabao 12 kwa msimu huu.

Kacheza mechi 14 akiwa ameyeyusha dakika 1,252 raia huyo wa Zambia chaguo la kwanza la Kocha Mkuu mzawa Juma Mgunda.

Mchezo ujao kwa Simba SC ni dhidi ya KMC unaotarajiwa kuchezwa Desemba 26, Uwanja wa CCM Kirumba katika mchezo uliopita walitoshana nguvu kwa kufungana mabao 2-2.

UNAWAZA KUHUSU JANUARY..? MERIDIANBET WANAKULETEA MCHONGO HUU MPYA…ZINGATIA HILI.. KWISHA KAZI….VIGOGO WAZITO YANGA SC WAITIBULIA AZAM FC KWA FEI TOTO…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply