Habari za Michezo
Habari za michezo

WAKATI AKIHAHA HUKU NA KULE…FIFA WAMPA TABASAMU AUSSEMS…..

admin December 27, 2022 7:34 am

KOCHA wa AFC Leopards, Patrick Aussems, amefurahishwa na urejeo wa wachezaji wake watano kwenye kikosi chake kutokana na kushindwa kuitumikia timu hiyo kufuatia kibano cha Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA).

Wachezaji 10 wa Ingwe hawajacheza mechi tatu za ufunguzi Ligi Kuu Kenya msimu huu wakisubiri maamuzi ya FIFA.

β€œUrejeo wa wachezaji hawa unaleta morale kwenye timu. Baadhi yao ni wazoefu na nina imani sasa tutanza kuandikisha matokeo mazuri. Ifikiapo Januari wachezaji wote watakuwa wamerejea kikosini tayari kupambana,” alisema Aussems kabla ya mchezo wao wa jana FKFPL dhidi ya Kakamega Homeboyz.

β€œNingependa pia kushukuru manejmenti ya timu ambayo imehakikisha kuwa mambo yamekuwa sawasawa kwenye timu.”

Wachezaji 10 ambao bado hawakujumuishwa ni pamoja na wale waliosajiliwa wakati wa dirisha la katikati la msimu wa 2021/22 na wengine waliopandishwa kutoka timu ya vijana ni Emmanuel Lwanga, Ronald Sichenje, Loren James, Victor Otieno, Aboubakar Musha, Nester Olum, Cliff Nyakeya, Josephat Lopaga, Victor Omune na Musa Oundo.

MKATABA WA SAIDO NA SIMBA SC KUFURU TUPU…NABI AWAKA YANGA SC….MAKAMBO ATUPIWA VIRAGO… ACHANA NA FEI TOTO…MWINGINE HUYU HAPA NAYE KAVUNJA MKATABA KISA PESA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply