Habari za Yanga
Habari za michezo

ACHANA NA FEI TOTO…MWINGINE HUYU HAPA NAYE KAVUNJA MKATABA KISA PESA…

admin December 27, 2022 7:37 am

KIUNGO wa Geita Gold, Yusuph Kagoma ameamua kuvunja mkataba wake wa miezi sita uliobaki ili kujiunga na Singida Big Star.

Nyota huyo aliyekuwa akiwindwa na Simba kwenye dirisha hili inaelezwa amefikia makubaliano binafsi na sasa anajiunga na walima alizeti hao.

Katibu Mkuu wa klabu hiyo, Liberatus Pastory alisema mchezaji atakayekwenda mezani kwao ili kuvunja mkataba kwa ajili ya maslahi yake wapo tayari kwani mchezo wa soka ni biashara.

“Hatuwezi kusema kwa sasa hivi kwamba ni nani ataondoka, lakini tupo kwenye mazungumzo na baadhi ya wachezaji wetu ambao mikataba imeisha au imebakisha miezi sita hivyo bado tunaendelea kupambana,” alisema Liberatus.

Katibu huyo aliongeza kuwa endapo mchezaji ataonyesha nia ya kuondoka kikosini hawatakuwa na pingamizi, bali watampa baraka zao.

Inasemekana kwamba tayari kiungo huyo amepewa baraka zote na viongozi na sasa yupo jijini Dodoma na timu hiyo iliyoweka kambi kwa ajili kujiwinda na mchezo wa kesho wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Dodoma Jiji.

Kagoma alijiunga na timu hiyo akitokea Gwambina na kusaini mkataba wa miaka miwili ambao hata hivyo ameamua kuuvunja.

Usajili wa Kagoma ni wa tatu dirisha hili kwa Singida Big Stars baada ya awali kumnasa beki, Nickson Kibabage kutoka Mtibwa Sugar na Ibrahim Ajibu aliyetokea Azam.

WAKATI AKIHAHA HUKU NA KULE…FIFA WAMPA TABASAMU AUSSEMS….. A-Z JINSI SIMBA SC WALIVYOWEKA REKODI HII MPYA JANA …CHAMA KAPITILIZA AISEE…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply