Home Habari za michezo HII NI KIMYA KIMYA AISEE…NINJA KARUDI YANGA SC KUOKOA JAHAZI…ISHU NZIMA IKO...

HII NI KIMYA KIMYA AISEE…NINJA KARUDI YANGA SC KUOKOA JAHAZI…ISHU NZIMA IKO HIVI…

Ninja arudi Yanga SC

Baada ya beki wa kati Abdallah Shaibu ‘Ninja’ kumaliza mkataba wake wa mkopo Dodoma Jiji, amerejea Yanga SC na ameanza rasmi mazoezi na wenzake kwenye Uwanja wa Avic Town, uliopo Kigamboni, Dar es Salaam.

Ninja alikuwa aungane na wenzake juzi Jumanne, lakini ilishindikana ambapo timu hiyo ilifanya mazoezi ya gym na jana ilifanya ya uwanjani ambapo ndipo aliungana nao rasmi kuanza kukiwasha, ikijiandaa na mechi dhidi ya Mtibwa Sugar itakayopigwa Manungu, Jumamosi, pia wakianza maandalizi kwa ajili ya Kombe la Mapinduzi.

Chanzo cha ndani cha uhakika kilisema kurejea kwa Ninja ndani ya kikosi hicho, anaweza akaendelea na timu hadi mkataba wake utakapomalizika mwishoni mwa msimu huu na pia kama atataka kwenda kwa mkopo kwingine watakaa mezani kujadili ili kulinda maslahi ya mchezaji na kocha wa timu hiyo anataka kumtumia kwenye Kombe la Mapinduzi.

“Ninja aliongeza mkataba wa mwaka mmoja kabla ya kwenda Dodoma Jiji, ambako mkopo wake ulikuwa unaishia dirisha hili dogo, ndio maana amerejea kwenye kikosi chake ili kuungana na wenzake,” kilisema chanzo ndani ya Yanga SC.

“Kama itahitajika aende kwa mkopo tena yatafanyika mazungumzo kwani bado ni mchezaji wetu, ila atafanya mazoezi na wenzake timu ikijiandaa na dhidi ya Mtibwa Sugar na Kombe la Mapinduzi.”

Chanzo hicho kilisema Ninja ni beki mzuri na wanaamini akipewa mechi nyingi zitamjengea kujiamini na kumrejesha kwenye makali kama alivyokuwa mwanzo ambapo alikuwa anatumika mara kwa mara.

“Angekuwa beki mbaya asingeweza kupata dili nje kipindi kile ambacho alikwenda kucheza Czech timu ya Daraja la Tatu ya MFK Karvina, hivyo Yanga SC inamtazama kwa jicho la tatu na isitoshe alisumbuliwa na majeraha kipindi fulani hadi akafanyiwaa upasuaji, hivyo asingeweza kurudi kwa kasi,” kilisema chanzo hicho.

Alipomtafuta Ninja alijibu kwa ufupi: Nani kakwambia? niache kwanza nikupigie kesho asubuhi.”

‘Ninja’ ni miongoni mwa wachezaji wachache waliopata bahati ya kucheza nnje ya nchi lakini hakuweza kuwa na muendelezo mzuri hali iliyopelekea kurudisha majeshi nchini, ambapo alijiunga tena na Yanga SC.

SOMA NA HII  KUHUSU KUKOSOLEWA NAMNA ANAVYOCHEZA....MUTALE KAWAPA JIBU HILI SIMBA...