Frank Domayo ajiunga na Namungo FC
Habari za michezo

DOMAYO ATUA ‘KITASHA’ NAMUNGO FC…STEPHEN SEY NAYE NDANI AISEE…

admin December 30, 2022 9:04 pm

Kiungo wa zamani wa Klabu ya Young Africans na Azam FC Frank Domayo ‘Chumvi’ ametambulishwa rasmi na Klabu ya Namungo FC ya mkoani Lindi.

Domayo amejiunga na klabu hiyo akiwa mchezaji huru, baada ya kuachwa na Azam FC mwishoni mwa msimu uliopita 2021/22.

Domayo ametambulishwa rasmi Klabuni hapo kupitia Kurasa na Mitandao ya Kijamii ya timu hiyo, huku taarifa hiyo ikiandikwa:

#WelcomeTosouthernkillers✅ Karibu kwenye Familia ya Namungo Fc Frank Raymond Domayo #Chumvi @domayo #southenkillers

Kiungo huyo anakuwa mchezaji wa pili kutambulishwa katika timu hiyo katika kipindi hiki cha Dirisha Dogo la Usajili, akitanguliwa na Mshambuliaji kutoka nchini Ghana Stephen Sey.

Sey aliwahi kuitumikia Namungo msimu wa 2020/21 kabla ya kuondoka, baada ya kusajiliwa na Klabu ya Eastern Company SC ya nchini Misri.

RAGE NAYE AJITOSA SAKATA LA FEI TOTO NA YANGA SC…KATEMA NONDO SIO POA… BIGIRIMANA NAYE AISHIKA PABAYA YANGA SC…KOCHA MPYA SIMBA AFICHWA ‘USHUANI’ HUKOO…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply