Home Habari za michezo FT: YANGA SC 3-0 POLISI TZ….MAYELE KAANZA UPYAAAA KUWATETEMESHA…HUYU MZINZE NI WA...

FT: YANGA SC 3-0 POLISI TZ….MAYELE KAANZA UPYAAAA KUWATETEMESHA…HUYU MZINZE NI WA ULAYA KABISA YANI…

MABINGWA Watetezi Yanga SC wameanza mzunguko wa pili kwa ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Polisi Tanzania mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania bara uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Mabao ya Yanga yamefungwa na Jesus Moloko dakika ya 46,Fiston Mayele dakika ya 77 na Clement Mzinze dakika ya 85.

Kwa ushindi huo Yanga wamefikisha Pointi 41 na kuendelea kuongoza katika msimamo wa Ligi hiyo nafasi ya pili wapo Azam FC wakiwa na Pointi 36 na Simba SC wakibaki nafasi ya tatu wakiwa na Pointi 34 wakiwa na mchezo mmoja Mkononi.

Mchezo mwingine umepigwa uwanja wa Sokoine jijini Mbeya weneyeji Tanzania Prisons wamefungwa mabao 2-1 na Singida Big Star.

Ligi hiyo itaendelea kesho Wekundu wa Msimbazi Simba watashuka katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza kucheza na wenyeji Geita Gold .

SOMA NA HII  GAMONDI AISHTUKIA SIMBA MAPINDUZI CUP ....AWAITA MASTAA WOTE ALIOWATOSA DAR...