Home Habari za michezo PAMOJA NA KUIFUNGA STARS, UGANDA WAJITOA CHAN…HUENDA TZ IKAPATA ‘NGEKEWA’…

PAMOJA NA KUIFUNGA STARS, UGANDA WAJITOA CHAN…HUENDA TZ IKAPATA ‘NGEKEWA’…

Timu ya Taifa ya Uganda ‘The Cranes’ imejiondoa kushiriki Fainali za Mataifa Bingwa Barani Afrika ‘CHAN’ zitakazorindima mapema mwaka 2023 nchini Algeria.

Uganda ilipata tiketi ya kushiriki Fainali hizo kwa kuifunga Tanzania ‘Taifa Stars’ mabao 4-0, baada ya michezo ya nyumbani ya ugenini.

Rais wa Shirikisho la soka Nchini Uganda ‘FUFA’ Moses Magogo amesema sababu kubwa ya kujitoa katika Fainali hizo ni kutokana na ukata wa fedha unaowakabili kwa sasa.

Tayari Uganda imeshatuma barua CAF ya kujiondoa kwenye Michuano hiyo, ambayo imepangwa kuanza kuunguruma Januari 13 hadi Februari 04 mwaka 2023.

Uganda imepangwa Kundi B lenye timu za DR Congo Ivory Coast na Senegal.

Endapo CAF wataridhia ombi la waganda kujitoa, huenda nafasi hiyo ikawaangukia Tanzania ambayo ilifungwa na Uganda kwenye mechi ya Mwisho ya kuwania kufuzu fainali hizo.

SOMA NA HII  SAMATTA ATAMBA KRC GENK...ANAKIWASHA BALAA...MAGOLI NA PASI USISEME