Home Habari za michezo TETESI: KISA MKWANJA ANAOKUNJA AL AHLY….SIMBA WAAMUA KUMPOTEZEA MAZIMA LUIS…

TETESI: KISA MKWANJA ANAOKUNJA AL AHLY….SIMBA WAAMUA KUMPOTEZEA MAZIMA LUIS…

Tetesi za Usajili Simba

Yule kijana mwenye mbio, Luis Miquissone yuko mtaani kwao Maputo. Ni hapo Msumbiji. Simba wamethibitisha itashindikana kumrudisha Msimbazi wakati huu wa usajili.

Viongozi wamekiri kutambua shauku ya mashabiki lakini baada ya kufanya naye mazungumzo wamekubaliana wamuache tu aendelee na ishu zake maana mshahara wake ni zaidi Sh120 milioni.

Mmoja wa viongozi wa usajili wa Simba amesema kuwa wanamtaka mchezaji huyo, lakini hawataweza kumchukua.

Baada ya kutolewa kwa mkopo na Al Ahly ya Misri kwenda Abha, Saudi Arabia alidumu kwa miezi michache na kurejea Maputo. Lakini dau analopewa Arabuni ni kubwa na Simba hawatamudu kulisogelea.

“Ametuambia wakala wake kuna masuala ya kimkataba wanayafuatilia Al Ahly kama yatamalizika kuna dili lingine kubwa la pesa ndefu amelipata zaidi ya hili la Simba. Katuonyesha mpaka ushahidi. Tukaamua kuachana naye akatengeneze maisha yake maana tumeishi naye vizuri,” alisema kiongozi huyo akiomba kutotajwa jina kwa madai safari hii wanafanya ishu zao kimyakimya.

“Miquissone wakati yupo Al Ahly alikuwa anapata zaidi ya Sh120 milioni kwa mwezi sio mwaka. Hiyo timu anayoweza kwenda atachukua mshahara karibu na kiasi hicho.”

Alisema kwa sasa wanasaka wachezaji kama Luis ili kuongeza nguvu dirisha dogo na wako tayari kutumia fedha, lakini sio kwa mshahara wa zaidi ya Sh100 milioni wa Luis.

Miquissone alitolewa kwa mkopo Abha kwa sababu ilikuwa inafundishwa na kocha wake wa zamani Simba, Sven Vandenbroeck.

Simba pia inaendelea kusaka kocha mpya na ina majina kadhaa mezani ambayo wiki ijayo watafanya uamuzi wa mwisho. “Kocha mpya wa Simba kama mambo hayatakwenda tofauti wiki ijayo tunaweza kumaliza mchakato na tukakubaliana naye ila anatokea Ulaya kwani Afrika imeshindikana kumpata,” alisema kiongozi huyo.

“Makocha wa Afrika wazuri kama tunawahitaji wapo wawili Pitso Mosimane au Florent Ibenge ambao kila mmoja kwenye timu yake kwa mwezi analipwa si chini ya Dola 100,000 zaidi ya Sh230 milioni, ambayo kiuhalisia kwetu Simba sio rahisi kutoa hiyo.”

SOMA NA HII  YANGA:- "KILICHOTUPELEKA ROBO FAINALI NI MKWANJA..."WACHEZAJI HAWALIPWI MAWE