Home Habari za michezo WAKATI MAMBO YAKIZIDI KURINDIMA QATAR… HIVI NDIVYO TANAPA WANAVYOENDELEA KUIPAISHA TZ

WAKATI MAMBO YAKIZIDI KURINDIMA QATAR… HIVI NDIVYO TANAPA WANAVYOENDELEA KUIPAISHA TZ

Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania kwa kushirikiana na taasisi nyingine za wizara ya Maliasili na Utalii (TTB, TFS) na kituo cha uwekezaji Tanzania -TIC limefanikiwa kutangaza vivutio vya utalii na fursa za uwekezaji zilizopo nchini katika sekta mbalimbali.

Wageni kutoka mataifa mbalimbali waliofika nchini Qatar kwa ajili ya mashindano ya kombe la Dunia, wameweza kupata taarifa muhimu kwa karibu na kwa urahisi kabisa, zinazohusu vivutio vinavyopatikana Tanzania, huduma muhimu na njia za kuwafikisha.

Aidha, Mheshimiwa Mahadhi Juma Maalim, Balozi wa Tanzania nchini Qatar alipata nafasi ya kukutana na washiriki wa maonesho haya na kufanya kikao kilichojadili masuala ya kuendeleza utangazaji wa vivutio vyetu ikiwemo kuwa na vipeperushi vya lugha ya kiarabu ambayo ndiyo inatumika zaidi nchi hapa.

Aidha, ofisi ya ubalozi pia iliwakutanisha washiriki na wawekezaji walionesha nia ya kuwekeza nchini na kufanya nao mazungumzo. Ili kuongeza wigo wa matangazo na uhamasishaji, washiriki kwa kushirikiana na ofisi ya Ubalozi, tumeweza kuratibu na kupata wanahabari ambapo Mh. Balozi aliweza kuzungumzia masuala mbalimbali yahusuyo utalii wa Tanzania na uwekezaji.

Katika maonesho haya, Tanzania ni nchi pekee kutoka Africa iliyopewa nafasi ya kuwa na banda. Nchi nyingine zinazoshiriki ni Korea, Marekani na Uturuki.

SOMA NA HII  MANARA:- YANGA TUNACHEZA STAILI YA 'PPP'.....'APOROMOSHA MVUA YA MANENO' KWA NABI....