Habari za Simba
Habari za michezo

‘SHOW’ YA NTIBAZONKIZA YAMUIBUA MAYELE…AFUNGUKA NAMNA ALIVYOKOSHWA…

admin January 1, 2023 8:07 pm

Juzi mshambuliaji wa SimbaΒ  SC ya Dar es Salaam, Saido Ntibazonkiza alianza kwa kishindo kuichezea timu hiyo akifunga mabao matatu katika ushindi wa mabao 7-1, ambao Simba SC iliupata dhidi ya Prisons.

Mara moja baada ya kuona kiwango cha Saido katika mchezo huo uliofanyika Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam, mshambuliaji wa Yanga, Fiston Mayele amesema Saido anastahili pongezi.

Kupitia Akaunti yake ya Instagram Mayele ameandika: β€œHongera sana Saido, mchezaji mkubwa ni mkubwa.”

Kwa upande wake Saido ambaye huo ulikuwa mchezo wake wa kwanza tangu ajiunge na Simba SC amesema anapambana kuhakikisha anasaidiana na wenzake kufikia malengo ya timu hiyo ifikapo mwishoni mwa msimu na anajisikia mwenye furaha kuanza vizuri kibarua chake kipya, akiwa na timu kubwa Simba .

Licha ya mabao hayo, Saido alihusika na bao moja lililofungwa na John Bocco ambaye naye alifunga mabao matatu katika mchezo huo.

FEI TOTO ‘AWAJAMBISHA’ YANGA SC…APANGA KUFUNGUKA YOTE …. SIRI YA AZIZI KI YAFICHUKA YANGA…FEI TOTO ATAJWA KUHUSIKA…KOCHA MBRAZILI SIMBA KUJA NA..

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply