Tetesi za Usajili Yanga
Habari za michezo

FEI TOTO ‘AWAJAMBISHA’ YANGA SC…APANGA KUFUNGUKA YOTE ….

admin January 1, 2023 7:54 pm

Kiungo Feisal Salum Abdallah (Fei Toto) asubuhi ya juzi Alhamis Disemba aliichezea timu yake ya zamani JKU kwenye mchezo wa Kirafiki dhidi ya Mlandege kwenye Uwanja wa Mao Zedong ambapo JKU walifanikiwa kupata ushindi wa Mabao 4-2.

Katika mchezo huo Fei alicheza dakika 45 za kipindi cha pili ambapo wakati anaingia Fei JKU walikuwa tayari wapo nyuma kwa Mabao 2-0, lakini baada ya kuingia Fei JKU wakafanikiwa kusawazisha Mabao hayo na kuongeza mengine mawili huku Fei akifunga 1 kati ya Mabao hayo 4 na akiwa na msaada mkubwa wa kupatikana mabao hayo.

Mwandishi wa Habari hii alifanya jitihada ya kuzungumza na Fei mara baada ya kumalizika mchezo huo lakini Fei aliomba kutozungumza chochote. “Naomba nisiongee chochote, naomba sana, ikifika siku ya kuongea nitaongea “. Alisema Fei.

Si mara va kwanza Fei kuonekana kucheza JKU kwani ndio Timu yake ya zamani aliyoondoka mwaka 2018 kabla ya kujiunga na Yanga.

SIMBA SC WAIBUKA NA MSIMAMO WAO KUHUSU DILI LA MANZOKI NA LUIS… ‘SHOW’ YA NTIBAZONKIZA YAMUIBUA MAYELE…AFUNGUKA NAMNA ALIVYOKOSHWA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply