Home Habari za michezo WAKATI FEI TOTO AKIONEKANA DUBAI….YANGA SC WAIBUKA NA KUTOA MSIMAMO HUU…

WAKATI FEI TOTO AKIONEKANA DUBAI….YANGA SC WAIBUKA NA KUTOA MSIMAMO HUU…

Fei toto atimka Yanga SC

Wakati Fei Toto akionekana Dubai, Rais wa Yanga SC Hersi Said  alipata kufanya mahojiano maalum na Azam TV na kuwatoa hofu wana Yanga SC kuwa hakuna mchezaji muhimu atakayeondoka Yanga SC kwa sasa.

Hersi amefika mbali na kueleza kuwa hata Feisal Salum hawezi kuondoka sababu bado ana msimu mmoja na nusu hadi 2024 lakini kingine hawezi kuondoka mchezaji yoyote sababu ya wana negotiations power (Nguvu katika mapatano).

“Kama club kwanza nataka niwahakikishie hakuna mchezaji mzuri ataondoka Yanga, tufute kwenye akili zetu hakuna mchezaji ataondoka Yanga katika utawala wetu ambaye sisi tunamuhitaji abaki” amesema Hersi

“Feisal mkataba wake unaisha 2024 bado yupo sana ana msimu huu ana msimu ujao halafu Feisal ni moja kati ya wachezaji muhimu kwenye kikosi chetu” >>> Hersi VIA Azam TV

SOMA NA HII  FT: USM 0-1 YANGA....WAMEKUFA KIBABE...NABI AMWAGA CHOZI HADHARANI...MAYELE , DIARRA WAWEKA HISTORIA...