Habari za Yanga
Habari za michezo

WAKATI BONGO WAKIMPONDA….MAYELE ASEPA KWAO CONGO…ISHU IKO HIVI…

admin January 4, 2023 7:39 pm

MSHAMBULIAJI kinara wa Yanga SC, Fiston Mayele ameifuata tuzo yake DR Congo ambayo inatarajiwa kutolewa Januari 7 mwaka huu.

Mayele ameondoka jioni hii kuelekea nchini kwao ambapo safari yake ni maalum kwaajili ya kushughulikia hati yake ya usafiri lakini pia ameweka wazi kuwa atasubiri na tuzo yake.

Mayele amesema amefurahia kupewa heshima na nchi yake kwa kumchagua kuwa mchezaji bora wa nchi yake.

“Ninafuraha na nathamini hiki walichokifanya wananifanya niongeze juhudi zaidi ya kupambana nikijua kunawatu wananifuatilia na kuthamini kile ninachokifanya,” amesema na kuongeza;

“Nitakuwa huku hadi Januari 8 ambapo nitaanza safari ya kurudi nchini Tanzania kuungana na timu kwaajili ya kuendelea na majukumu ya timu.”

KIMYA KIMYA…TAMBWE ATUPIWA VIRAGO SINGIDA BIG STARS…ISHU IKO HIVI… SAKATA LA FEI TOTO KUITEMA YANGA SC…ABDI KASSIM KAIBUKA NA HILI LA KWAKE…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply